MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI - DKT.SAMIA
MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI - DKT.SAMIA
# Asema baada ya Vijiji vyote Meatu kupata umeme kasi inaelekea vitongojini
# Ataka umeme utumike kuongeza thamani ya mazao, kilimo na ufugaji
Simiyu
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassani amesema Serikali imeendelea kupeleka maendeleo katika Wilaya ya
Meatu ikiwemo ukamilishaji wa usambazaji umeme katika Vijiji vyote 109
vya Wilaya hiyo.
Dkt. Samia ameyasema hayo Juni 17, 2025 Wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu akiwa kwenye ziara ya kikazi.
"Kama
tulivyoahidi, hatujaishia hapo, kazi ya usambazaji umeme sasa
inaendelea kwenye vitongoji lakini pamoja na jitihada hizi zote
ninafahamu kuna changamoto ya umeme kutokuwa na nguvu ambayo
inatatuliwa." Amesema Dkt. Samia
Ameeleza
kuwa, Wizara ya Nishati inatatua changamoto hiyo ya umeme kutokuwa
na nguvu kwa kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Shinyanga hadi
Simiyu na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme.
Amesema
kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea uwepo wa umeme wenye nguvu na wa
kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo Viwanda.
Amesisitiza
kuwa, lengo la Serikali ni kuona wananchi wanatumia nishati ya umeme
kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani ya mazao, kilimo na
ufugaji.




No comments