WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA AFUNGUA MKUTANO WA 73 WA ACI AFRICA
WAZIRI MKUU AWASILI ARUSHA AFUNGUA MKUTANO WA 73 WA ACI AFRICA .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wadau mbalimbali wa viwanja vya ndege wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege kwa Ukanda wa Afrika (ACI Afrika) unaofanyika jijini Arusha
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akziungumza kuhusu jukwaa hilo adimu linalowaleta pamoja viongozi na wasimamizi wa usafiri wa anga, waendeshaji wa viwanja vya ndege kujadili na kubadilishana mawazo katika kuboresha na kuikuza sekta ya usafiri wa Anga.
Rais wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege kwa Ukanda wa Afrika (ACI Afrika) Emanuel Chaves akizungumzia mafanikio endelevu sekta ya anga afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege kwa Ukanda wa Afrika (ACI Afrika) unaofanyika jijini Arusha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akizungumzia mipango mbalimbali ya wizara katika kukuza usafiri wa Anga hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo akizungumzia fursa mbalimbali zilizopo kwenye viwanja vya ndege wakati wa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege kwa Ukanda wa Afrika (ACI Afrika) unaofanyika jijini Arusha.
Na. Vero Ignatus Arusha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Christian Makonda pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Chama leo tarehe 28 Aprili, 2025.
Waziri Mkuu amesema hayo (Aprili 28, 2015) wakati akifungua Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la viwanja vya ndege kwa kanda ya Afrika (ACI Afrika) unaofanyika kwenye Hotel ya Mount Meru kuwa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Anga.
Amesema kuwa moja ya eneo ambalo Rais Dkt. Samia ameendelea kusimamia ni ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege nchini ikiwemo ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha msalato kilichopo jijini Dodoma, uboreshaji wa viwanja vingine vya kimkakati vya Kilimanjaro, Unguja, Pemba, Mwanza, Kigoma, Tabora, Shinyanga na Sumbawanga.
“Pia tunaendeleza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti unaolenga kukuza utalii wa mazingira huku tukihifadhi mfumo ikolojia wa Serengeti, Kadhalika Uwanja wetu wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere umefanikiwa kushinda Tuzo ya Usalama ya Baraza la Viwanja vya Ndege Duniani, katika viwanja vyenye miruko ya ndege 50000 kwa mwaka”alisema
Vile vile Waziri Mkuu amesema kutokana na jitihada za Serikali za kuiimarisha Sekta ya anga, Tanzania imetajwa na Shirika la ICAO kushika nafasi ya nne Barani Afrika kwenye masuala ya usalama wa anga,ambapo imewekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya mawasiliano kwenye viwanja wa ndege na masafa marefu ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa ndege na abiria.
Akizungumzia kuhusu shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Waziri Mkuu amesema hivi sasa ndege zake zinatoa huduma ya usafiri katika viwanja 15 vya ndani na nje ya nchi katika nchi za Dubai, Mumbai, Guangzhou, Johannesburg, Nairobi, Harare, Lusaka, Entebe na Kinshasa
“Shirika pia linatarajia kuongea safari zake katika miji ya London, Lagos, Accra, Juba, Muscat na maeneo mengine ya masoko ya kimkakati ili kuiunganisha Tanzania Kikanda na Kimataifa”
Kwa Upande wake, Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa mkutano huo inatoa jukwaa adimu linalowaleta pamoja viongozi na wasimamizi wa usafiri wa anga, waendeshaji wa viwanja vya ndege kujadili na kubadilishana mawazo katika kuboresha na kuikuza sekta ya usafiri wa Anga.
Naye Rais wa Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika Emmanuel Chaves amesema kuwa sio tu kwenye utungaji wa Sera bali kwenye maamuzi tunayoyafanya sasa katika kushirikiana “Kama tutaamua kwa dhati tutajenga Afrika yenye muunganiko na ushindani katika sekta ya anga”
Pia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo ametoa shukrani kwa wadau mbalimbali waliofika katika mkutano huo wenye tija hasa katika ukanda wa Afrika.
Awali akitoa salamu kwa mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda Arusha amemshukuru Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
kwa kuridhia uwanja huo mzuri wa kisasa katika mkoa wa Arusha ambapo unaweza ukawa namba moja basi ama namba mbili katika nchi ya Tanzania .
Vile vile ameshukuru Prof. Godius Walter Kahyarara Katibu Mkuu wa Wizara kwa kuridhiwa uwanja huo kutumika kwa ndege ndogo zinazounganisha Afrika ya Mashariki kwa wageni wanaotaka kutua katika uwanja huo
"Nafahamu hatua zinaendelea vizuri na siyo muda mrefu Mamlaka watatangaza ya kwamba Arusha unaweza kutumia sasa uwanja wa ndege kama point of interest na kuwaruhusu wageni wenye private jet kuja Arusha bila kuhangaika kwenda Kilimanjaro. Alisema Makonda
"Nafahamu hatua zinaendelea vizuri na siyo muda mrefu Mamlaka watatangaza ya kwamba Arusha unaweza kutumia sasa uwanja wa ndege kama point of interest na kuwaruhusu wageni wenye private jet kuja Arusha bila kuhangaika kwenda Kilimanjaro. Alisema Makonda.
Pia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo ametoa shukrani kwa wadau mbalimbali waliofika katika mkutano huo wenye tija hasa katika ukanda wa Afrika






No comments