RC BALOZI BATILDA BURIANI AWATAKA WANANCHI WOTE WA TANGA KUHUDHURIA BILA KUKOSA SIKU TISA ZA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA LEGAL AID
RC BALOZI BATILDA BURIANI AWATAKA WANANCHI WOTE WA TANGA KUHUDHURIA BILA KUKOSA SIKU TISA ZA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA LEGAL AID
Wananchi pamoja na Wakazi wa mkoa wa Tanga wameaswa kushiriki Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ya siku tisa itakayofanyika kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga kuanzia Aprili 8 hadi
Kupitia kampeni hiyo, wakazi hao watapata elimu na huduma kwa masuala mbalimbali yanayohusiana na sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt. Batilda Burian, ametangaza kufanyika kwa kampeni hiyo, ikijumuisha halmashauri 11 za Mkoa huo.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, huduma zitakazotolewa ni pamoja na elimu ya masuala ya kisheria kama haki za binadamu, na
Nyingine ni utawala bora, ndoa, mirathi, migogoro ya ardhi, pamoja na usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kutoka RITA, na usajili wa vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA.
Amesema zaidi ya wataalamu 40 kutoka taasisi mbalimbali za sheria, wamewasili mkoani humo kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.
Mhe Balozi Dkt. Batilda amesema, kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria, na kuimarisha ushauri wa kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia,.
Pia kutakuwa na kusaidia kutatua migogoro mingi ya muda mrefu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, wazee wa jadi, na viongozi wa dini.
Kwa upande wake, Mratibu wa kampeni hiyo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Laurent Burilo, amesema wamefanikiwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2 katika mikoa 23, na kutatua zaidi ya migogoro 4,000. Amehimiza wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kwani migogoro mingi inaweza kumalizwa ndani ya siku moja au mbili kupitia msaada huu wa kitaalamu.
No comments