KONGAMANO LA SIKU TATU LA WAFAWIDHI WA MATUKIO (Washereheshaji)KUFANYIKA ARUSHA AICC
Mwl.Bryceson Makena ni muasisi wa Kisima amefafanua kuwa kongamano hilo la siku tatu litakuwa na zaidi ya washiriki 1000
KONGAMANO LA SIKU TATU lA WAFAWIDHI WA (Washereheshaji )KUFANYIKA ARUSHA AICC
Na.Vero Ignatus,Arusha
Chama cha wafawidhi wa matukio nchini Tanzania (KISIMA CHA MAFANIKIO ) wameandaa kongamano la kuongeza uelewa na maarifa juu ya tasnia nzima ya ushehereshaji itakayoanyika Jijini Arusha kuanzia Aprili 12-14 katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb)Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mwl.Makena amesema kwa kutambua juhudi za serikali chini ya Rais wa Tanzania Dkt Samia, kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana, kumomonyoko wa maadili na janga la kukosa uzalendo,amesema wao kama wadau wa tasnia husika wameamua kuunga juhudi hizo kwa vitendo kwa kuelimisha ,kuhamasisha,kuburudisha ,kushauri pamoja na kujifunza sera ,miongozo,maelekezo,mipango mikakati na vipaumbele vya kitaifa kupitia majukwaa tunayowasiliana moja kwa moja na jamii kubwa ya watanzania kwenye shughuli na matukio wanayoratibu .
“Chama chetu kina zaidi ya wanachama 450 waliogawanyika kanda 6,na bado tunaendelea kupokea wanachama wapya,mfawidhi wa matukio mmoja anaweza kukutana na watu zaidi ya 1000 kwa wiki katika matukio mawili tofauti ya muda wa kazi na baada ya kazi kwa mwezi anakutana nawatu 4000,fani hii inahitaji mafunzo rasmi na vyeti vya kitaalam tofauti na kauli zilizozoeleka mtaani kwamba vijana wengi wanaingia kwenye fani kwasababu ni kazi rahisi sana ati mdomo haulipi VATna hakuna gharama kubwa ya kuendesha kazi hii zaidi ya kuwa na suti tatu nne,kitu ambacho kinashusha hadhi ya,heshima na thamani ya taaluma’’alisema Makena.
Ester Kimweri ni mwenyekiti wa Kisima cha Mafanikio amesema hadi sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 75 amesema wameamua kufanya kongamano hilo Arusha ili wapate pia wasaa wa kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi za taifa.
‘’Sisi ni Washereheshaji tutakapofika hifadhini kwanza kunachangia pato la Taifa ,pia tunayofursa ya kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo katiika hifadhi zetu kwa kupitia kurasa zetu mbalimbali za kijamii,vilevile pale tunapopata wasaa tukiwa kwenye utendaji kazi wetu wa kila siku’’alisema Esta.
Akizungumza mmoja wa wanachama wa Kisima cha Mafanikio Bi Happyness Mushi amesema kuwa kabla hajajiunga na chama hicho alikuwa ni mshehereshaji asiyejua namna ya kupangilia shughuli zake,ila baada ya kujiunga amenufaika na Elimu ambayo inatolewa marakwamara amejifunza namna bora ya kuratibu matukio mbalimbali katika shughuli za kijamii,kiserikali kwa kuzingatia itifaki
Vilevile amesema kuwa anaiomba serikali kupitia barazaza la sana Mashirikisho mengine mbalimbali kuwatambua wafadhili matukio kwa kuwatupia jicho lapilli kama vile kwa wasanii mbalimbali wa filamu,vichekesho,wanamuziki
Aidha Kisima cha mafanikio ni chama kilichosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2020 chini ya sheria ya Jumuiya ya 337 kwa usajili Na.SA 21669 ili kujishughulisha na nyanja za kitaaluma,kijamii kiuchumi na kitamaduni,vilevile kinatambuliwa na Wizara ya Habari ,Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa kwa Sheria Na.23 ya mwaka 1984 na kupewa kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa Nchini Na.BST-9684-190
No comments