RC MAKONDA AUNGANA NA WATAALM, MADAKTARI KUMCHANGIA MAMA AMBAYE AMEENDA KUTIBIWA MOI

RC MAKONDA AUNGANA NA WATAALM, MADAKTARI KUMCHANGIA MAMA AMBAYE  AMEENDA KUTIBIWA MOI

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda ameungana na wataalamu wa Afya wakiwemo Madaktari wauguzi pamoja na watoa huduma kumchangia fedha za matumizi Mama ambaye mtoto wake anaenda kutibiwa katika taasisi ya mifupa ya Moi jijini Dar es Salaam

Fedha hizo kiasi cha Milioni 1.3 zimetolewa katika hafla ya chakula cha usiku kwa wataalamu hao wa sekta ya Afya na Mkuu huyo wa mkoa na kukabidhi kwa Mganga mkuu wa mkoa Charles Mkombachepa ili zikamsaidia Mama huyo na Mwanaye wakati wa matibabu  jijini Dar es salaam

Mtoto huyo ni miongoni mwa wagonjwa zaidi ya elfu 32 waliopata matibabu kwenye kambi ya Madaktari bingwa na wabobezi iliyofanyika kwa takribani juma moja kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha ambapo imeelezwa kuwa mama wa mtoto huyo alilazimika kuomba msaada wa kuchangiwa nauli kutoka mkoani Mbeya hadi Arusha kwa ajili ya kufuata huduma hiyo

No comments