MADAKTARI 50 WATUA ARUSHA KUONGEZA KASI KAMBI YA RC MAKONDA.
MADAKTARI 50 WATUA ARUSHA KUONGEZA KASI KAMBI YA RC MAKONDA.
Jumla ya Madaktari 50 kutoka kwenye mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara na Kilimanjaro wamewasili Mkoani Arusha alfajiri ya leo na kuanza rasmi majukumu ya kuwahudumia wananchi kwenye kambi maalum ya matibabu inayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Charles James Migunga, Mratibu wa Tiba mkoa wa Arusha amewaambia wanahabari kuwa amewapokea madaktari hao mapema leo Juni 27, 2024 ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda aliyoyatoa jana katika jitihada za kuboresha na kuongeza kasi kwenye utoaji wa huduma za afya.
Katika hatua nyingine pia, Mratibu huyo wa tiba Mkoa wa Arusha amesema serikali ya Mkoa imeongeza maeneo ya kutolea huduma za vipimo na matibabu, yote hayo yakiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Paul Christian Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Leo Alhamisi Juni 27, 2024 ni siku ya nne ya Kambi maalum ya Matibabu yenye lengo la kutoa elimu, vipimo na matibabu bure kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha ambapo takribani watoa huduma na madaktari bingwa na wabobezi 500 wanatoa huduma katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
No comments