ZAIDI YAWAGENI 2000 KUSHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WAHASIBU WAKUU WA SERIKALI BARANI AFRIKA
Na.Vero
Ignatus,Arusha
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu
wa kimataifa wa wahasibu,wakaguzi wa hesabu,wataalam wa masuala ya
fedha,Tehama,vihatarishi na kada nyingine wakiwemo walioajiriwa
serikalini,kampuni binafsi pamoja na waliopo katika ajira binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi
wa Aicc Jijini Arusha Mhasibu Mkuu wa serikali CPA Leonard Mkude amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa na
washiriki zaidi ya 2000,ambapo utawaleta pamoja wahasibu wakuu wa serikali
Afrika watakaoambatana na wahasibu wakuu wa wizara ,Taasisi za umma ,wahasibu
na wadau wengine .
‘’Wahasibu
na wakaguzi wa hesabu watakaohudhuria watapata fursa ya kusikiliza mada za
masuala mbalimbali ya kitaaluma pia kukutana na wahasibu wakuu wa serikali wa
Afrika na kubadilisha na mawazo kupeana mawasiliano na kujua fursa
zinazopatikana katika nchi za frika’’.alisema Mkude.
Mkude amesema kuwa mkutano huo utaafanyika nchini
kuanzia tarehe 2 hdi 5 Disemba mwaka 2024 katika kituo cha mikutano cha kimatifa Arusha (AICC)huku lengo
la mkutano huo likitajwa kuwa ni Kujenga Imani katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma
kwa ukuaji Endelevu.
‘’Ujo
huo wa wageni kutoka nje wataleta fedha za kigeni mbazo watazitumia hapa nchini
Tanzania katika kuunga mkono dhamira ya Rais ya kutangaza utalii wa Tanzania kwani
wageni hawa watatembezwa katika mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali’’ alisema
CPA Mkude.
Ameainisha faida mbalimbali za mkutano huo kuwa ni pamoja
na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji jumuishi na maendeleo
endelevu,Bara jumuishi lililoungnishwa kisiasa na kwakuzingatia maadili,Afrika
yenye utawala bora,Amani na Usalama,Utambulisho thabiti wa kitamaduni,urithi wa
pamoja maadili yanayoshirikishwa.
Akizungumza Mwenyekiti wa wa Umoja wa wahasibu wakuu wa Afrika ndugu Mahehlohonolo Mahase amesema kuwa hawachachagua kwa bahati mbaya mkutano huo ufanyike Nchini Tanzania kwasababu ni nchi kinara katika matumizi sahihi ya mifumo,pia mshirika mwaminifu wa umoja huo,vilevile kuna vivutio vingi vya utalii na watu wengi wamekuwa wakisikia tu hivyo wanatamani kuja kuyaona yale ambayo wamekuwa wakiyasikia.
Mahase
amesema kuwa umoja wao ni mzuri ambao unalenga kuzisaidia nchi wanachama katika
masuala mazima ya kutafuta rasilimali fedha na kuangalia namna gani
rasilimalifedha hizo zitatumika katika maendeleo ya nchi husika.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha AICC Christine Mwakatobe alisema kuwa wamejipanga vilivyo kuwapokea wageni wa mkutano mkuu wa pili wa wahasibu wakuu wa Afrika na kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora huku wakitegemea kwamba wageni watakapoondoka watarudi tena kutokana na huduma waliyoitoa kwao.
Mwakatobe amemshukuru Dkt Samia kwa kazi kubwa
aliyoifanyaa kwani yeye ni mwanadiplomasia namba moja ambao umezaa matunda
makubwa kwani wameona mikutano mingi inakuja kwenye kumbi zao ,vilevile utalii
umeongezeka pamoja na wawekezaji wameongezeka,pamoja na fursa mbalimbali
zilizopo.
Aidha Umoja huo wa wahasibu wakuu wa serikali Afrika ulizinduliwa rasmi Mombasa ,Kenya tarehe
5 julai 2023 bada ya azimio la kufunga umoja wa wahasibu uliokuwepo katika
kanda mbalimbali kwa sasa nchi 55 za umoja wa Afrika ni mwanachama wa Umoja
huo.
No comments