YALIKUWA MAKUSUDI YA MUNGU, MAKONDA KULETWA ARUSHA"- DORAH

"YALIKUWA MAKUSUDI YA MUNGU, MAKONDA KULETWA ARUSHA"- DORAH

Bibi Dorah Belita Mollel Mwenyeji wa Arusha amemshukuru Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda kwa kuwakumbuka na kuwatetea wanyonge katika kuhakikisha kuwa wanapata haki na huduma muhimu za kijamii ambazo walikuwa wakizikosa kutokana na umaskini walionao.

Bibi Dorah Belita aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la Macho pamoja na nyonga kwa zaidi ya miaka saba sasa, ametoa shukrani hizo mara baada ya kupata matibabu na kupatiwa miwani kwenye kliniki maalum ya madaktari bingwa iliyoingia siku yake ya nne leo kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Bibi huyo mnufaika wa Kambi ya matibabu na wiki ya haki iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda amesema anaamini kuwa Mwenyenzi Mungu amemleta Arusha kwa Makusudi Mhe. Makonda, na amemuombea kheri na nguvu zaidi kutokana na namna ambavyo amekuwa akifika kwa urahisi pamoja na kuamsha uwajibikaji kwa watumishi wengine wa Mkoa wa Arusha tangu kuteuliwa kwake.

No comments