MAONYESHO YA 4 YA Utalii yafanyika mkoani Kilimanjari
Na Vero Iganatus ,Kilimanjaro
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alizungumza katika maonyesho hayo yaliyofanyika chuo cha ushirika Moshi.
Mkurugenzi wa Kilifair Dominick Shoo akaizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya nne ya kulifair
Na Vero Iganatus ,Kilimanjaro
Maonyesho ya
Kimataifa ya Utalii ya (KaribuKilifair )yamezinduliwa rasmi leo na Waziri a Utali
na maliasili Hamisi Kigwangala katika uwanja wa chuo cha ushirika wilayani Moshi
mkoani Kilimanjaro yakiwa ni ya nne ambapo zaidi ya makampuni 4000 kutoka
duniani yameweza kushiriki.
Kigwangala amewapongeza Karibufair pamoja na
Kilifair kwa kuunganisha matamasha hayo
mawili ya kutangaza vivutio vya utalii nchini amabapo amesema hakuna ushindani
wa ndani bali na ushirikiano bali upo ushindani wa nje.
Amesema mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka 5 unaelekeza
mambo kadhaa kwenye sekta ya utalii,ikiwemo kuboresa mazingira ya kufanya
biashara,leseni ya wakala wautalii amabapo serikali imerahisisha kutengeneza
dirisha moja la kuoza tozo mbalimbali,dirisha la kodi,kurahisisha usajili wa
biashara pia utoaji wa vibali mbalimbali
Katika
jitihada hizo amesema mambo kadhaa yamefanyika likiwemo ya uzitazama baadhi ya
tozo na kuziondoa ,kama ile ya TALA leseni ya wakala wa utalii,amabapo serikali
imeshusha tozo sawa na shilingi za kitanzania sawa na dola 200 hadi dola 500
‘’Dola hizi
500 ni kwa kampuni amabayo itkuwa na magari kati ya 1hadi3,kwa hiyo ukiwa na gari moja safari hii
unaweza kuingia tofauti na zamani ilikuwa lazima uwe na magari matano”alisema
Kigwangala.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa Kilifair bwana Dominick Shoo amesema kutokana na mjumuiko wa
maonyesho hayo watahakikisha kuwa kila mkoa shiriki unapata stahiki yake ya
kifedha nakisapot kutoka katika maonyesho hayo
Shoo ametoa
sababu kwanini kiingilio ni shilingi 8000 ,amesema dhumuni kubwa haswa wanahitaji watu ambao wanaweza kufanya
biashara katika maonyesho hayowakiwa na lengo maonyesho yasiwe na watu wengi
amabao hawana sababu za msingi bali aweze kupata fursa ya kujifunza biashara
Aidha amesema
katika makubaliano yao waliamua kwamba kipindi kijacho maonyesho hayo yatafanyika mkoani Arusha
No comments