BASI LAGONGA TRENI KIGOMA MJINI....KUNA TAARIFA YA VIFO..ANGALIA PICHA
Habari tulizozipata kutoka mkoani Kigoma asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018 ni kwamba basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa linatoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Editha Karlo anasema ajali hiyo imetokea leo alfajiri, mpaka sasa idadi ya vifo na majeruhi bado haijajulikana,Tutawaletea taarifa kamili hivi punde

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa












No comments