HIACE YAGONGANA NA LORI LA MCHANGA NA KUUA WATU 14 MKURANGA
Habari tulizozipata hivi punde zinasema watu zaidi ya 10 wanasadikiwa kufarikiki dunia kwa ajali iliyotokea leo Juni 25,2018 saa 10 alfajiri Mkuranga baada ya gari la mchanga kugongana na Hiace iliyokuwa inatoka Mkuranga kwenda Dar es salaam.
Mwenyekiti na mjumbe wa kitongoji cha Dungani ilipotokea ajali hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali na polisi wamefika eneo la tukio.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Dungani Mohammed Ngota amesema watu 14 wamefariki dunia huku majeruhi wakiwa wanne wakiwemo watoto wawili.


No comments