Uzinduzi wa Albam ya Afadhali ya Mjengoni Classic Band wafana Arusha,Uzinduzi huo wapambwa na mwanamama Saida Karoli

Na.Vero Ignatus ,Arusha

Mjengoni Classic Band imezindua albamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la Afadhali yenye jumla ya nyimbo saba katika ukumbi wa Mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha

Uzinduzi huo ulipambwa na mwanamziki mkongwe kutoka Bukoba Saida Karoli,ambapo Bandi hiyo ya Mjengoni Classic ilikuwa inatimiza mwaka mmoja ,na ndiyo albamu yao ya kwanza yenye jumla ya nyimbo (7)

Bendi hiyo yenye jumla ya wanamuziki 17wanawake (2)na wanaume15,kati ya hao wapigaji vyombo ni 6 na waimbaji 11

Akizungumzia malengo ya bendi hiyo kwa ujumla mkurugenzi mwenza wa Band hiyo Emmanuel Babu amesema kuwa kutoa burudani kwa wakazi wa Arusha na vitongoji vyake kwa Watanzania na kuvuka mipaka kwenda nje ya nchi.

Amesemakuwa wao wanawalea vijana na wanatoa mafunzo muziki kwa vijana kutambua vipaji vyao hadi sasa wameshatoa mafunzo hayo kwa vijana 13 na wanaendelea vizuri
Baadhi ya waimbaji wa Mjengoni Classic Bandi wakiwa jukwaani katika uzinduzi wa albamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la Afadhali.

Mpiga bass gitaaa Fujo bass  akifanya yake katika uzinduzi wa albamu yao mpya katika ukumbi wa mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha.

Mpigaji wa Ryizim gitaa Mjengoni Classic Band  Aridi siku ya uzinduzi .

Mwimbaji wa Mjengini Classic Band Jures akiimba katika uzinduzi huo.

Muimbaji wa Mjengoni Classic Band Dany Star akiimba katika uzinduzi huo katika ukumbi wa mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha.

Waimbaji wa Mjengoni Classic Band Jonico akiimba katika uzinduzi huo katika Ukumbi wa Mjengoni Club uliopo Olasiti Jijini Arusha.
Mwanamuziki Saida Karoli akiwa anatumbuiza katika Uzinduzi wa Albamu ya kwanza ya Mjengoni Classic Bandi,katika Ukumbi wa Mjengoni Club iliyopo Olasiti Jijini Arusha.Picha kwa hisani ya Vero Ignatus Blog.

Mpiga Kinanda Baraka wa mjengoni Classic Band akifanya yake katika Uzinduzi wa alabamu yao inayojulikana kwa jina la Afadhali katika ukumbi wa Mjengoni Classic Band uliopo Olasiti  Jijini Arusha.

Wacharaza magitaa la solo na rizimu wakifanya yao katika uzinduzi huo Jijini Arusha .Rythim gitaa wa kwanza kushoto Aridi akifuatiwa na Sele akiwa anapiga gitaa la solo.
Mpiga solo wa bendi ya Mjengoni Classic Sele akifanya yake katika uzinduzi wa albamu yao ijukikanayo kama Afadhali ,
Mwanamama JaneCindy akiimba katika uzinduzi wa albamu ya Mjengoni classic band ikiwa pia imetimiza mwaka mmoja
Mpiga drums wa mjengoni Classic Band Peter Drums katika uzinduzi wa albanmu ya mjengoni Classic Band ijulikanayo kwa jina la Afadhali



















No comments