KIHAMIA Amsimamisha kazi Afisa Usafirishaji wa Jiji la Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athman Kihamia amemsimamisha kazi Afisa Usafirishaji wa Jiji Edward Moriko kwa Uzembe na kumteua Frank Sanga kukaimu nafasi hiyo kwa muda.
Akizunguzungumza mara  baada ya kutembelea eneo la maegesho ya Magari ya Jiji (Depot) Ngarenaro Kihamia amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na kushindwa kusimia kitengo chake Ipasavyo.

Aidha ameongeza kuwa Afisa huyo ameshindwa kutoa taarifa Polisi mara baada ya kutokea Ajali ya Magari mawili ya Halmashauri hiyo pamoja na kuajiri Madereva bila kufuata utaratibu.

Kihamia amekiri kuwa kuna changamoto ya upungufu wa Madereva lakini tayari wametoa taarifa ya kuomba kibali cha kuajiri na muda sio mrefu tatizo hilo litakwisha mara moja

No comments