ARUSHA: Askari Magereza Arusha amuua askari mwenzie kwa risasi
Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia Askari Magereza Faustin Massanja kwa kumpiga risasi na kumuua askari mwezake Ombeni Mwakiyani wa Magereza kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi baina yao.(ugomvi wa kimapenzi)
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa uchunguzi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo la kupigwa risasi kwa askari magereza
Akizungumza na waandishi wa habari mtu wa karibu na askari hao amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa askari hao ni wivu wa mapenzi ambapo marehemu pamoja na mtuhumiwa ambaye ametambulika kwa jina la Faustine Masanja wamepanga nyumba moja.
Amedai marehemu alipofika asubuhi kazini ndipo mtuhumiwa Masanja alimpiga mwenzake risasi ya kichwa na alipokimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru alifariki dunia.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha hilo na kusema tukio hilo limetokea asubuhi wakati askari hao wakiwa kazini na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa Mount Meru.
Aidha Kamanda Mkumbo amedai kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi
No comments