TANZIA: MWANAHABARI JOYCE MMASI AFARIKI DUNIA

MWANDISHI wa Habari Mkongwe, Bi. Joyce Mmasi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 6, 2017 jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinasema Bi. Mmasi alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya TMJ ilioko Mikocheni jijini Dar es Salaam akipatriwa matibabu kwa mudsa kidogo.
Marehemu wakati wa uhai wake, amewahi kuandikia magazeti ya Majira na Mwanchi.
Aidha katika mawasiano yake ya mwisho na mwandishi mwingine, Hellen Mwango anayetumia jina la (Mwene Nataha) wiki iliyopita kwenye ukurasa wa Facebook, Mmasi aliandika. "
"Naumwa Mwene wew mkubwa mwenzangu siko bedrest ila naumwa njoo TMJ gorofa ya kwanza tutaongea"maneno yako ya mwisho Joyce Mmasi uliyoniandikia kwa njia ya whatsapp sikupata muda wa kuja Mama sikubahatika kuja kikusikiliza mpenzi wangu tangulia Joyce.Namshukumuru Mungu tu sina la kusema watoto wako Joyce wangu! ðŸ˜ŠðŸ˜ŠðŸ˜ŠðŸ˜ŠðŸ˜Štangulia Mama.
Habari Zaidi kuhusu msiba wa mwanahabari huyo zitawajia kadiri zitakavyotufikia

No comments