Balozi Dkt. Kasiluka:Ndoto ya Dkt.Samia ni Kuwa na Mashirika Yenye Ufanisi na Ubora

Balozi Dkt. Kasiluka:Ndoto ya Dkt.Samia ni Kuwa na Mashirika Yenye Ufanisi na Ubora 
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu akisoma maazimio sita yaliyoazimiwa na viongozi katika kikao kazi Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa taasisi na Mashirika ya Umma kilichofanyika jijini hapa kuanzia  Agosti 27 hadi 30,
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Mbaga Kida
Na. Vero Ignatus Arusha. 

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameanisha  jumla ya maazimio sita yaliyoazimiwa na viongozi katika kikao kazi Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa taasisi na Mashirika ya Umma ikiwemo, Ushiriki katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2050 na uandaaji wa mipango mkakati wa taasisi za umma;  Utawala bora na mawasiliano ya umma pamoja na Usimamizi wa rasilimali watu, mafunzo na uendelezaji wa uongozi bora.

Mchechu amesema Maazimio mengini ni, Mikakati ya taasisi na mashirika ya umma kuwekeza nje ya Tanzania; Kuongeza uchangiaji na kupunguza utegemezi katika Mfuko Mkuu wa Taifa na kutekeleza kikamilifu maazimio yaliyotolewa kwenye kikao kilichopita ambayo hayajatekelezwa.

Akifunga kikao kazi hicho kilichofanyika jijini hapa kuanzia  Agosti 27 hadi 30, 2024. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amesema kuwa ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha nchi inakuwa na mashirika yenye ufanisi mkubwa na wa viwango vya kimataifa.

Hivyo, amewataka Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa taasisi na Mashirika ya Umma kuhakikisha wanatekeleza kwa ukamilifu maagizo yaliyotolewa na Mhe. Rais Samia.

"Serikali itayachukua maazimio yote yaliyokubaliwa na nawaahidi yatafanyiwa kazi, tutawasaidia kuhakikisha yanatekelezeka ili kutimiza ndoto ya Mhe. Rais Samia juu ya taasisi na mashirika ya umma", amesema Balozi, Dkt. Kusiluka.

Amewataka viongozi wa taasisi na mashirika ya umma kujenga utamaduni wa kujifunza mbinu na  mikakati mipya kutoka kwa mashirika yaliofanikiwa na kuitazama serikali kwa upana wake.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Mbaga Kida amesema kuwa wamewasilisha malengo na wanaamini watayasimamia  malengo hayo ili kuweza kuhakikisha yale waliyojiwekea katika kusimamia na kuboresha utendaji kazi wa taasisi na mashirika ya umma yanaweza kufikiwa.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba, Kamishna wa Bima Tanzania kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania,  Dkt. Baghayo Saqware amesema kuwa Wakuu wa Taasisi wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi na wanaahidi kuyatekeleza kwani wana hamu na mageuzi yanayotarajiwa.

No comments