TAKUKURU YATOA PONGEZI KWA RC MAKONDA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.
TAKUKURU YATOA PONGEZI KWA RC MAKONDA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU) Kupitia kwa Mkurugenzi wake Mkuu Bw. Chrispin Francis Chalamila leo Ijumaa Septemba 13, 2024 imetoa pongezi maalum kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa kutambua mchango wake mkubwa katika mapambano dhidi ya rushwa Mkoani Arusha. Pongezi hizo zimeambatana na makabidhiano ya Ngao ya TAKUKURU kama ishara ya kuenzi jitihada zake katika kutokomeza vitendo vya rushwa Mkoani Arusha.
Ngao aliyokabidhiwa Mhe. Makonda imebeba Ujumbe usemao "Kuzuia rushwa ni Jukumu langu na lako, tutimize wajibu wetu."
No comments