DKT. MPANGO AFUNGUA JUKWAA LA 24 NA MKUTANO WA 35 WA UNFCCC MKOANI ARUSHA
DKT. MPANGO AFUNGUA JUKWAA LA 24 NA MKUTANO WA 35 WA UNFCCC MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na viongozi na washiriki mbalimbali wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 35 wa Kamati ya Kudumu ya Fedha ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Tarehe 02 Septemba 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki katika U
DKT. MPANGO AFUNGUA JUKWAA LA 24 NA MKUTANO WA 35 WA UNFCCC MKOANI ARUSHA
Màkamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amesema Jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 2.2 zilizokusanywa katika Kongamano la Nishati Safi ya Kupika huko Paris, Mei 2024 ili kusaidia nishati safi.
Makamu wa Raisi amesema hayo ni maendeleo ya kutia moyo ambayo yatasaidia katika kukabiliana na changamoto za kimazingira,kiafya, kijamii na kiuchumi zinazohusiana na matumizi ya nishati ya jadi ya kupikia.
Ameyasema hayo Leo 02 September Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa kimataifa 35 wa kamati ya kudumu ya fedha ya mkataba wa Umoja wa mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi(UNFCCC).
Mkutano huo unaozishirikisha nchi 80 kutoka mataifa mbalimbali ambao ni kikao kuelekea Mkutàno wa Cop 29,2024 nchini Indonesia wenye Kaulimbiu ya mkutano huo isemayo , "Kuongeza kasi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhili unaozingatia Jinsia"
Amekumbusha umuhimu wa usawa katika kukabiliana na masuala ya mabadiliko ya tabianchi, akisema Tanzania imeendelea kuhimiza ujumuishaji wa masuala ya jinsia na mabadiliko ya tabianchi kwenye sera, programu na mikakati yake katika ngazi mbalimbali za kiuongozi.
,
Dkt.Mpango amesema lengo ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Tanzania yote inakuwa na miyeyusho safi ya kupikia, kutoka asilimia 7 ya sasa.
"Kwa kuwa tunahitaji mabadiliko ya haki ambayo yanazingatia jinsia, tunapendekeza kwamba upishi safi uwe mojawapo ya maeneo ya kuzingatia katika COP29 huko Baku"Alisisitiza Makamu wa raisi.
Naye Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,Dk,Ashati Kijaji alsema mabadiliko ya hali ya hewa hutuletea hatari kubwa, zinazojidhihirisha kupitia hali mbaya ya hewa, kupanda kwa joto, mvua zisizobadilika, dhoruba za kitropiki na mafuriko makubwa, kila moja ikiathiri uchumi na mfumo wa ikolojia wa jamii .
Alisema changamoto hizo husababisha hasara kubwa na uharibifu wa miundombinu muhimu, kutoka kwa barabara na madaraja hadi huduma na njia za umeme pia zinatishia huduma muhimu zinazotegemea maisha na kusababisha uhaba wa maji , chakula.




No comments