MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO JUKWAa LA 24 NA MKUTANO WA 35 WA KAMATI YA KUDUMU YA FEDHA



MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO JUKWAa LA 24 NA MKUTANO WA 35 WA KAMATI YA KUDUMU YA FEDHA

Na. Vero Ignatus,Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip 
Isdor Mpango, Septemba 02, 2024 anatarajiwa kufungua Jukwaa la 24 na 
Mkutano wa 35 wa kamati ya Kudumu ya Fedha ya Mkataba wa Umoja wa 
Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, ( UNFCCC, standing Commitee on 
Finance) katika kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha (AICC).

Mkutano huu unatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 02- 06, 2024,na kuhudhuriwa na Washiriki 200
kutoka Nchi zaidi ya 80 duniani ikiwa ni 
mara ya kwanza kwa mkutano wa aina hii kufanyika nchini Tanzania ambapo ni 
Maandalizi ya Mkutano wa COP29 unaotarajiwa kufanyika Novemba,11-
22,2024 Baku,nchini Azerbaijan. 

Aisha Kufanyika kwa mkutano huo nchini Tanzania ni kutokana na ombi la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliomba United Nations Framework
Convention on climate change (UNFCCC) kuruhusu kamati yake ya fedha kuja 
kufanya mkutano huo muhimu ambao utawezesha upatikanaji wa fecha za 
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kamati ya kudumu ya fedha ni moja ya kamati chini ya Mkataba wa Umoja wa 
Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi iliyoundwa katika mkutano wake wa 16 
wa Nchi Wanachama (COP16).

Lengo la kamati hiyo ni kuwezehsa upatikanaji wa fecha za utekelezaji wa shughuli za mkataba. Kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 32 waliochaguliwa kutoka Nchi zinazoendela na zilizoendelea ambazo ni wanachama wa mkataba huo.

Mkutano huu wenye kauli mbiu “Kuongeza kasi katika Kukabiliana na 
Mabadiliko ya Tabianchi kupitia Ufadhili Unaozingatia Jinsia”.. 
 

No comments