Tanzania imepanga kuzalisha megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2030
Tanzania imepanga kuzalisha megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Msaidizi Maalum wa Rais wa Marekani wa Masuala ya Uhifadhi wa Mazingira, Fedha na Uvumbuzi, Bw. Nana Ayensu amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa nchi washiriki katika kufungua milango ya uendelezaji wa nishati ya nyuklia ambayo ni rafiki kwa matumizi ya binadamu na hifadhi ya mazingira na pia kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi husika.
Ameongeza kuwa nishati ya nyuklia itafanikisha ajenda za kimataifa za nishati safi zinazoendelea ikiwemo nishati safi ya kupikia inayopigiwa chapuo kimataifa huku kinara wake akiwa ni Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumzia utayari wa nchi yake, amesema Marekani ipo tayari kushirikiana na nchi za Afrika ili kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia ambayo inatoa uhakika wa upatikanaji nishati na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

No comments