TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA YAASWA KUTAFUTA NJIA ZITAKAZOWAWEZESHA KUWEKEZA NJE YA NCHI
TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA YAASWA KUTAFUTA NJIA ZITAKAZOWAWEZESHA KUWEKEZA NJE YA NCHI
Na. Vero Ignatus Arusha
Ofisi ya Msajili wa hazina imesema kuwa hadi sasa ya lo jumla ya mashirika ya Umma 248 huku mashirika yasiyokuwa ya Umma yakiwa 58 ambapo jumla ya uwekezaji huo ni Shilingi trillion 73 ambapo amezitaka kujikita katika njia mbalimbali zitakazowawezesha kuwekeza nje ya nchi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Taifa
Hayo yamesemwa na Nehemiah Mchechu ambaye ni Msajili m wa hazina alipokuwa akizungumza na waandishi kuelekea kikaokazi cha jukwaa la wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za serikali (CO'S Forum 2024) ambapo mutant huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan jumatano 28,2024
Kwa upande mwingine, Mchechu ameeleza kuwa hii ni mara ya pili kufanyika kwa kikao hicho na anatarajia ndani ya miaka mitatu kitakuwa cha mafanikio zaidi ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025, taasisi na mashirika ya umma kati ya 30 hadi 40 yatapunguza utegemezi kwa kuanza kujitegemea, vilevile yataweza kutoa gawio kwa serikali.
Mchechu alisema kuwa Taasisi zilizochangia mwaka wa fedha uliomalizika ziliongezeka kutoka Taasisi 109 hadi kufikia 145 ambapo Taasisi 36 ziliongezeka, hivyo ni matumaini yao kwamba mwaka huu wa fedha unaoanza watakwenda kuwa na Taasisi nyingi zaidi
Aidha amesiaitiza kwamba tulio hilo kwao ni muhimu kwani viongozi hao wanakutana kubadilishana uzoefu sambamba na kuweka mikakati ya pamoja kwani ni wait ambao wananafasi kubwa ya kusimamia uchumi wa Taifa.
"Unapoangalia uchumi wa nchi ndani ya serikali unaitazama katika makundi mawili muhimu ikiwemo yale ambapo matumizi mengi yanafanyika, na kule ambapo uzalishaji unafanyika hivyo basi ndani ya serikali kazi zao ni kutengeneza Sera na kuzisimamia katika uzalishaji, Ila unaporudi katika uchumi wa nchi kuna mapato yatokanayo na Kodi na yale yasiyotokana na Kodi. Alisema
Katika kuyatendea kazi maagizo waliyopewa na Mhe. Rais mwaka wa fedha uliopita 2023,Mchechu amesema tayari kuna mabadiliko katika Taasisi za Umma katila utendaji wake, maboresho katika uendeshaji wa Taasisi hizo, ikiwa ni pamoja na kuwa pamoja baadhi yao Uhuru wa kujiendesha ambapo kwa sasa zipo Taasisi 48 zinafanya hivyo, pamoja na kuwasimamia upande wenye visa ndogo na kuhakikisha kuwa kuna ushirikishwaji m kubwa ambapo vikao vinaendelea, kuchangia Pato la serikali, pamoja na kutimiza wajibu wao.
Vilevie katika eneo la Kufanya mabadiliko ya kisheria utaratibu unaendelea kwani mabadiliko hayo yanakwenda kuzaa vitu vya msingi vitakavyosaidia mabadiliko ya kiuchumi pamoja na utendaji wa kazi wa taasisi za umma unatakiwa kubadilika ili kuwa na mawazo mapana yatakayowawezesha kuwekeza nje ya nchi.
Amesisitiza ili waweze kuona mabadiliko makubwa katika Taasisi hizo lazima kuwemo na mabadiliko ya namna ya kuweka uongozi imara na shupavu, upimaji wa ufanisi wa kazi katika Taasisi kwa kuzingatia vigezo vitano ambavyo ni pamoja na kuona namna gani wanachangia faida katika Pato la serikali, namna gani wanatumia rasilimali walizonazo, unawajibika vipi katika Mambo ya kisekta, utawala Bora, unaishi vipi na wafanyakazi wako, unawahudumia vip wateja wako
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa AICC Christine Mwakatobe aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandalizi yo te yamekamilika kwaajili ya Kikao kazi hicho cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma 2024
Kikao kazi hicho cha Wenyeviti wa Bodi ya watendaji wa Taasisi ya Umma kitafanyika Jijini Arusha tarehe 28/8/2024 kimebeba kaulimbiu isemayo Mikakati ya Taasisi na mashirika ya Umma kuwekeza nje ya Tanzania.
No comments