JAMII YAOMBWA KUUNGA MKONO MAPAMBANO YA KUMLINDA MTOTO WA KIUME DHIDI YA UKATILI WA ULAWITI

JAMII YAOMBWA KUUNGA MKONO MAPAMBANO YA KUMLINDA MTOTO WA KIUME DHIDI YA UKATILI WA ULAWITI
Baba Askofu Dkt Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikan akizungumza na Vijana katika kongamano la siku moja likiloandaliwa na Taasisi I siyo ya Kiserikali ya Vuka Initiative ambalo limebeba jina la Mlinde Mtoto wa Kiume dhidi ya Ukatili wa Ukawiti
Mkurugenzi wa Taasisi ya  isiyo ya Kiserikali Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus katika kongamano la siku moja lililobeba Jina la "Mlinde Motto was Kiume dhidi ya Ukatili wa Ulawiti"
Mkuu wa Dawati la Jinsia Kutoka Jeshi la Polisi SP Happiness Tem vijana wa Kiume hata kukiwepo na Shauri hata wakiitwa polisi hawaji wanadhana potofu kuwa Dawati linawahusu wanawake tu jambo ambalo siyo kweli kwani hata wao linawahusu
Habiba Madebe Mratibu wa Jinsia na Malezi ya Mtoto Kutoka Arusha Jiji
Dkt. Na mtaalam wa Afya ya Akili akizungumza katika kongamano likiloandaliwa na Vuka initiative katika Chuo cha Ufundi  Arusha. 
Baadhi ya washiriki wa kongamano la Mlinde Mtoto wa kiume dhidi ya ukatili wa ULAWITI lililojumuisha vijana wa kiume na baadhi ya wazazi katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC) . 
Baadhi ya washiriki wa kongamano la Mlinde Mtoto wa kiume dhidi ya ukatili wa ULAWITI lililojumuisha vijana wa kiume na baadhi ya wazazi katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC) . 
Na. Mwandishi wetu, Arusha

Kutokana na Watoto wengi wa Kiume kutosikilizwa mara nyingi wamekuwa wakitendewa ukatili hata baadhi yao wamekuwa wakitishiwa jambo ambalo limewafaya kukosa ujasiri wa kujieleza,huku wengi wao wamejikuta na kauli zisizokuwa na matumaini yeyote kwao, bila kusahau sehemu kubwa ya ukatili ukiwa unafanyika nyumbani. 

Akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya  isiyo ya Kiserikali Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus katika kongamano la siku moja julai 27/2024 lililobeba Jina la "Mlinde Motto was Kiume dhidi ya Ukatili wa Ulawiti" lililowakutanisha vijana wa kiume na mabinti zaidi ya 100 wazazi katika chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kuwa kampeni hiyo imekuja kutoka na  mmomonyoko wa maadili katika jamii na wazazi kukosa muda wa Kukaa watoto wao.

Aidha Bi Veronica amesema kwamba lengo kuu la kongamano hilo  ni kuwakumbusha Wazazi na Walezi kutambua umuhimu wao katika malezi na makuzi stahiki kwa watoto wa Kiume, kutambua changamoto za Ukatili wanazozipitia, sambamba na kuzitolea taarifa sehemu husika  ili kuhakikisga watoto hao wanakuwa salama, pamoja na kupatiwa maadili mema ili aweze kuja kuisimamia vyema familia yake. 

"Tumekuwa tukisikia/ kuona baadhi ya watoto wetu wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja na hii ni hali inayosikitisha,Mtoto wa kiume akishaharibiwa hawezi kusaidiwa tena,tunaomba wazazi walezi viongozi mbalimbali tutupie suala hili macho kwa karibu kuwanusuru watoto wetu WA Kiume kwaajili ya Familia na Taifa kwa ujumla. 

Aidha  Bi Veronica  amesema  Wazazi wamekua wakitumia muda mwingi kutafuta mali na kushindwa kumsikiliza mtoto wa kiume hivyo kupelekea kumnyima haki yake ya kumsikiliza, ukizingatia ukuaji wa Sayansi na Teknolojia pamoja na muungiliano wa mila na desturi hivyo baadhi ya wazazi wanakua wakali kupita kiasi,lakini pia kuna wazazi wanaowaachia watoto kila wanachokitaka hivyo kuwafanya watoto kubweteka mwishowe wanapokuwa watu wazima wanataka vitu kwa urahisi hatimaye anajiingiza kwenye vitu visivyofaa. 

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika kaongamano hilo Baba Askofu Dkt.Stanley Hotay amesema mtoto wa Kiume amekuwa akikataliwa katika Jamii, familia, shuleni hali inayompelekea kuchanganyikiwa na kutokufahamu asimame upande upi kwani amewekwa kuwa daraja la pili, hata wakati mwingine ameshindwa kufanya maamuzi ya busara kwasababu ya kukosa ujasiri. 

Amesema ili vijana hao waweze kuepukana  kutokana na janga lililopo la ushoga amewaomba viongozi wa dini mbalimbali, Wazazi walezi viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa kuungana kwa pamoja kutafuta mbinu mbadala ya kuwanusuru watoto wa Kiume katika changamoto iliyopo kwa sasa ili kupata Taifa Bora. 

Kwa upande wake mkuu wa Dawati la Jinsia kutika Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha  SP Happiness Temu amesema kuwa vijana wa Kiume hata kukiwepo na Shauri hata wakiitwa polisi hawaendi kwasababu wanachukulia kwamba Dawati linawahusu wanawake na siyo wao. 

"Hii inatokana na mazingira aliyolelewa, Mila na desturi ambazo zinamuonyesha mtoto wa Kiume hapaswi kusema pale anapoumizwa, kupigwa au kufanyiwa ukatili  wa kulawitiwa ama kubakwa , kwamba italeta aibu katika Jamii yao jambo ambalo siyo sawa,kwani Mtu yeyote ana haki ya kusema pale anapotendewa ukatili wa aina yeyote. 

Aidha kongamano hilo limebeba ujumbe usemao mimi ni chimbuko la Familia,Mimi ni Kichwa cha Familia Mimi ni Kiongozi ajaye ,Nilinde nisilawitiwe ,huku kaulimbiu ikiwa ni Jenga msingi bira kwa mtoto wa Kiume kwa manufaa ya Taifa Lijalo



No comments