Wafugaji hakikisheni mnafuata kanuni na taratibu bora za kifugaji

Champlick Dairy hii humsaidia ng'ombe kuongeza maziwa. 
Meneja masoko kutoka kampuni Animal care Mwinyimkuu Suleiman wanaojihusisha na kutengeneza chakula cha wanyama na kuku akitoa elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini katika viwanja vya TASO Njiro Arusha. 

Na. Vero Ignatus. ARUSHA

Wafugaji nchini wametakiwa kufuata kanuni na taratibu bora za  kifugaji sambamba na kufahamu vyakula vyenye virutubisho vya kutosha kwa wanyama husika.


Mnyama anahitaji chakula chenye uwiano wa nguvu, wanga, na mafuta, protini, madini, na vitamini kwani huo ndiyo msingi thabiti wa kuzalisha maziwa mengi

Mtaalam kutoka kampuni ya kutengeneza vyakula vya mifugo  Dkt. Henest Mwanga amesema kuwa maji ni kiungo muhimu kwa mifugo kama vile binadamu anavyoshauriwa kunywa maji kwa siku, ndivyo yanansaidia mnyama kutengeneza maziwa kutokana na chakula wanachokula. 
Chakula cha mbwa chenye madini, vitamini, protini yenye mlo kamili kwa mbwa. (champdog). 

Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Animal care Mwinyimkuu Suleiman asema kuwa wao wanajishughulisha na usambazaji na utengenezaji wa chakula cha kuku wa mayai, wanyama, kutoka vifaranga hadi wanakua. 

Pia wanayengeneza madini ya ng'ombe, chakula cha mbwa na gulukosi kwaajili ya vifaranga. 





No comments