Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji akizungumza katika mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI)
Picha na Vero Ignatus.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha.
Wapili kutoka kushoto ni Naibu waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, aliyepo kulia kwake ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware, akifuatiwa na Rukia Adam Mjumbe kutoka (TIRA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka baadhi ya matataifa 39 Duniani. Picha na Vero Ignatus.
|
Na.Vero Ignatus.Arusha
Mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda
wa makampuni ya Bima kutoka nchi 39 za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI)
umefunguliwa leo rasmi mkoani Arusha.
Mkutano huo
umefunguliwa na Naibu waziri wa fedha Dkt. Ashatu Kijaji ambapo
ameyataka makampuni ya Bima kutoa huduma za Bima kwa wakulima ili
kufikia uchumi wa kati.
|
|
| Dk, Kijaji amesema asilimia 75 ya
Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu kuhusu bima ikiwemo kupata
mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika
uchumi wa kati. |
Ameyataka makampuni ya bima nchini
kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa
wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima
nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima.
Amesema watanzania wanaotumia
bima hapa nchini ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi
kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa ofisi ya
Takwimu za Taifa.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa
BIMA nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware amesema mkutano huo wa 41 unatoa fursa
kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje za bima
zinavyofanya kazi kwa ufanisi.
Aidha amesema kampuni hizo zitapata
fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta
mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima, rasilimali watu na
kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya
maisha.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman amesema lengo la mkutano huo ni
kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote
ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi
za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima.
Mwisho.
No comments