RPC -Manyara ataka vijana kushiriki vita dhidi ya Ujangili na uhifadhi
Babati Manyara
Vijana wilayani Babati mkoa wa Manyara, wametakiwa kushiriki katika vita dhidi ya ujangili na uhifadhi wa Mazingira ili waendelee kunufaika mapato yatokanayo ya sekta ya Utalii.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine Senga, alitoa wito huo jana katika tamasha la kupiga vita Ujangili na uhifadhi wa Mazingira, liliandaliwa na Taasisi cha Chemchem wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Kamanda Senga alisema, ujangili sio tu, unapoteza rasilimali za nchi bali ni makosa ya jinai kwani tayari serikali imepiga marufuku uwindaji haramu.
"sisi sote hasa vijana tujuwe ni jukumu letu kupiga vita ujangili,kutunza mazingira na kuacha tabia ya kuvamia katika maeneo yaliyohifadhiwa na tukifanikiwa tutaendelea kupata faida kutoka sekta ya utalii"alisema
Hata hivyo, Kamanda Senga alieleza uwepo wa tamasha hilo kumesaidia kuwepo wa amani na utulivu kwa wananchi wa eneo hilo ambao wameunda jumuiya ya uhifadhi ya wanyapori ya jamii(WMA) ya burunge tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Awali Meneja Chemchem, Kanali mstaafu Leonard Werema, alisema taasisi yao ambayo inaendelesha hoteli za kitalii za chemchema na kitalu cha uwindaji, katika eneo la tarafa ya Mbugwe,imeona itumie tamasha kutoa elimu juu ya kupiga vita ujangili na uhifadhi wa mazingira.
"tunaamini kupitia tamasha kama hili, watoto wadogo,wanafunzi, vijana na watu wazima watapa elimu ya uhifadhi na kujua athari za ujangili"alisema
Alisema taasisi hiyo tangu mwaka 2014 imekuwa ikiandaa tamasha hilo kwa kukusanya vijana,wanafunzi na vikundi mbali mbali vya watu wazima, ili kupata elimu ya uhifadhi.
Akizungumza katika tamasha hilo, Mkuu wa wilaya ya Babati,Elizabethi Kitundu alisema serikali inaunga mkono jitihada za uhifadhi na kupiga vita ujangili ambazo zinaendelea wilayni Babati.
"leo ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, nimejifuza mengi nawapongeza Chemchem kwa kazi ya kutoa elimu ya kupambana na ujangili na kutunza mazingira na serikali tutaendelea kutoa ushirikiano"alisema.
Tamasha hilo, lilijumuisha ngoma za asili za kiberbeig, kimasai, kimbugwe na michezo ikiwepo soka na mpira wa pite ambapo zaidi ya milioni 20 zinatarajiwa kutumika.
MWISHO





No comments