TUME YA NGUVU YA ATOMIKI NCHINI WATOA ELIMU YA MIONZI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI NANENANE KANDA YA KASKAZINI


Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Yesaye Sungita, wa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo akiguatiwa na Mtafiti wa Tume hiyo Jerome Mwimanzi wakitoa elimu kwa mmoja wa mgeni aliyetembelea katika banda hilo katika maonyesho ya nane nane Kanda ya Kaskazini katika viwanja vya Themi Njiro Arusha. 


Na.Vero Ignatus -Arusha 

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji juu ya uthibiti wa viasilia vya mionzi vinavyoweza kupatikana kwenye mazao ya chakula na mifugo ili kuongeza usalama wa mtumiaji dhidi ya madhara hatari yanayosababishwa na mionzi.

Katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini  wanatoa elimu juu ya nyuklia inayoweza kuwa mkombozi kwenye ukuaji wa uchumi wa biashara na viwanda ikilenga matumizi salama teknolojia nchini ili kuboresha ustawi wa kwenye sekta ya afya,maji ,kilimo,nishati na mifugo.

Mtafiti wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Yesaya Sungita amesema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 30%ya vyakula duniani vinahribika kila mwaka kwa sababu ya kuharibiwa na na vijidudu au kuoza ,upotevu au kuharibika kwa chakula kuna athari kubwa katika kipato cha wakulima.

Aidha kila mwaka inakadiriwa hasara inayotokana na kuharibika kwa mazao ya nafaka barani Afrika haswa kusini mwa jingo la sahara inafikia dola za kimarekani bilioni 4 sawa na asilimia 15 ya thamani ya mavuno hayosambamba na matukio ya binadamu kuambukizwa vijidudu vya salmonella yanafikia iddi ya watu 120,000 kila mwaka ambapo maambukizi yamekuwa yakisbabisha vifo vingi.

 "Gharama ya matibabu yanayosababishwa na madhara ya maambukizi haya ya vijidudu vya salmonella na Ecoli yamekuwa yakisababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni 6 kila mwaka.alisema Yesaya" 

Afisa mawasiliano wa Tume Peter Ngamilo amesema Teknlojia ya nyuklia ina mchango mkubwa katika sekta ya kilimo na mazao ya mifugo kwani uhakiki bidhaa zitokananzo na mazao zinakuwa bora na za uhakika ili kuboresha afya ya mlaji .

Aidha katika hatua za awali tume hiyo imefanya upembuzi yakinifu wa kutumia teknolojia ya nyuklia /mionzi katika kuhifadhi chakula ,mazao na kuboresha bidhaa za viwandani ili kuzipa muda mkubwa wa matumizi na kuzikinga dhidhi ya haribifu unaoweza kusababishwa na bakteria.

Hivyo wananchi haswa wa Arusha na mikoa jirani  wameaswa kulitembelea banda la Tume ya nguvu za Atomiki ili wajipatie elimu juu ya huduma zinazotolewa sambamba na kujionea majukumu kisheria kwenye usimamizi na uthibiti wa mionzi nchini ili kulinda mazingira ,wananchi na wafanyakazi wanaotumia vyanzo vya mionzi katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

"Maonyesho hayo ya 25 ya kilimo na sherehe za nanenane mwaka 2018 kanda ya kaskazini yamebeba kauli mbiu isemayo" Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya Viwanda"

No comments