DKT. NGUVILA: ARUSHA WADAU WA MATUMIZI YA SERIKALI MTANDAO
Na. Vero Ignatus, Arusha
Sekta zote zinatumia mifumo ya kidijitali ya serikali
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Toba Alnason Nguvila amesema kuwa, mkoa wa Arusha ni wadau wa matumizi ya Serikali huku Taasisi zote za binafsi na Serikali mkoani huo, zikitumia mifumo ya kidijitali katika kutoa huduma kwa wananchi, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali na dhamira ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya kidijitali katika kutoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza kwenye Kikao cha sita cha Serikali Mtandao, kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha - AICC , leo Februari 19, 2026, Dkt. Nguvila amebainisha kuwa, Mamlaka ya Serikali Mtandao - eGA, ni wadau wa kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa Taasisi za Serikali nchini.
Amebainisha kuwa, Mkoa wa Arusha ni wadau wakubwa wa Serikali Mtandao, kutokana na kuwa Taasisi zote za Serikali mkoani humo, ni watumiaji wazuri wa mifumo ya kidigitali kwa kuzingati ndio sera na maelekezo ya Serikali.
"Kama tunavyofahamu, mwaka 2027, Arusha ni wenyeji wa mashindano ya Mpira wa Miguu Afrika - AFCON, hivyo ni wakati sahihi eGA kuja kuunganisha mifumo ya kidigitali, ili kurahisisha shughuli zote wakati wa mashindano ya AFCON, kwa kuwa tunategemea kuwa na wageni wengi wa ndani na nje ya nchi".Amesema Dkt.Nguvila.
Aidha, amesisitiza kuwa, Mkoa huo unaunga mkono jitihada za ssrikali za kuwa matumizi ya mifumo ya kidijitali, mifumo ambayo licha ya kurahisisha kazi imeondoa urasimu na kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika kuwahudumia wnanchi.
Hata hivyo Dkt. Nguvila ametumia wasaa huo, kuwashukuru Ega, kwa kuiamini Arusha na kuwa mwenyeji wa Kikao hicho kwa miaka sita mfululizo, sambamba na kuwakaribisha wageni wote kifurahia hali nzuri ya hewa ya Arusha huku akiwasisitiza kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za wanyama za Arusha, Manyara na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Awali, Kikao hicho, chenye Kauli Mbiu ya Kuboresha Utendaji wa Serikali kwa kuimarisha Utoaji wa Huduma za Umma kupitia Mifumo Salam a na Jumuishi ya Serikali Mtandao, kitafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 19 - 21 Februari, 2026.
https://www.instagram.com/p/DU3E6ODiPqZ/?igsh=YWFmaTRndWFuamhr
No comments