BALOZI DKT KUSILUKA: e-GA ZINGATIENI ULINZI NA USALAMA WA TAARIFA BINAFSI.

Na. Vero Ignatus,Arusha

BALOZI DKT KUSILUKA: e-GA  ZINGATIENI ULINZI NA USALAMA WA TAARIFA BINAFSI. 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, amefungua rasmi Kikao kazi cha sita cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) leo 17 februari 2026 jijini Arusha huku akitilia mkazo suala la kulinda usalama wa taarifa binafsi ambapo amezitaka  taasisi zote kuzingatia sheria na kujisajili kwenye taasisi ya ulinzi wa taarifa binafsi ili kuhakikisha zinahifadhiwa kwa usalama. 

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Kusiluka ameielekeza  e-GA kuwasilisha taarifa ya miradi yote ya TEHAMA Serikalini, ambayo haikuzingatia Sheria, Kanuni na Viwango vya Serikali Mtandao ili hatua zichukuliwe kwa wahusika kwa mujibu wa sheria,kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi wa TEHAMA, sambamba na 
 taasisi hizo kutangaza mifumo mbalimbali wanayobuni, ikiwamo teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence), ili ijulikane kwa wananchi na kuwasaidia kurahisisha shughuli zao za kila siku.

Dkt. Kusiluka amesema Kila Mkuu wa taasisi ya umma, anawajibika kuhakikisha miradi yote ya TEHAMA katika taasisi yake inazingatia takwa la kisheria mwaka 2019, Kanuni zake, Viwango na Miongozo yote ya Serikali kuanzia uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wake,pamoja na kufuata taratibu nzima zinazopaswa kufuatwa, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha andiko la mradi e-GA, kabla ya kuanzisha miradi hiyo.

Vilevile mewataka wataalamu wa TEHAMA kuwasaidia vijana kutumia mitandao kwa mambo yenye tija badala ya kujihusisha na matumizi hasi yanayoweza kuhatarisha usalama na amani ya nchi.
TEHAMA ni kipaumbele muhimu kwa Serikali ya Awamu ya Sita, hivyo nasisitiza huduma zake zipatikane kwa haraka na kwa urahisi, lakini pia ubunifu wowote utangazwe ili wananchi waweze kuelewa na kuutumia,” amesema Balozi Dkt. Kusiluka.

Nafahamu kuwa, ipo miradi ya TEHAMA ya Serikali inayojengwa kwa ushirikiano na
sekta binafsi, lakini hii haitoi kibali kwa miradi hiyo kukiuka sheria iliyowekwa.
Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini, mnafahamu
 Nawaelekeza kuzingatia sheria na taratibu
zilizowekwa, wale wote watakaokaidi sheria hili watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria. Alisema

Aidha amesema Mafanikio ya Tanzania kutambuliwa kimataifa kupitia tuzo za Umoja wa Mataifa (UN Public Service Award), World Summit on the Information Society (WSIS), na tathmini ya Benki ya Dunia ya GovTech Maturity Index, ni ushahidi kuwa nchi ya Tanzania ipo katika
mwelekeo sahihi wa mageuzi ya Kidijitali Serikalini,amwsema Mafanikio haya si ya e-GA pekee,bali ni ya Serikali yote na Watanzania kwa ujumla.

"Hii imefanya Nchi yetu kutambuliwa kimataifa kuoiga hatua za kimaendeleo na kupata tuzo ya Umoja wa mataifa ya ubunifu katika huduma UN Public Service innovation Award 2024kuoitia mofumo wa e-merejesho, tuzo ya Umoja wa mataifa ya (World summit on the information society) kupitia e-meejesho awamu ya pili
(emrejeshov2) ripoti ya ukuaji wa teknolojia duniani utoaji huduma za Serikali na ushirikishwaji wananchi Gov-Tech maturity index (GTM1) wa dunia 2025 ambapo Tanzania imeorodheshwa kundi A".Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Serikali Mtandao (eGa) Benedict Ndomba  katika hicho kilichudhuriwa na wajumbe 1400,wageni kutoka India Afrika ya Kusini ambacho kimebeba kaulimbiu isemayo kuboresha utendaji wa Serikali kwa kuimarisha utoaji wa huduma za umma kupitia mifumo salama na jumuishi ya  Mtandao ambapo mada 14 zitawasilishwa

Ndomba amesema kuwa Malengo ya kikao kazi hicho ni Kupanua wigo wa upatikanaji wa taarifa muhimu katika kila ngazi Serikalini, Kuimarisha usalama wa Serikali na raia wake katika karne ya sayansi na teknolojia na kuongeza uwezo wa Serikali kupambana na majanga kwa kutumia teknolojia ili kurahisisha michakato ya utendaji kazi kuanzia kwenye Wizara

Amesema pamoja na mafanikio hayo waliyonayo, bado kuna changamoto kadhaa zinazopunguza ufanisi wa utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao ikiwemo uhaba wa wataalamu wabobezi wa TEHAMA katika maeneo mbalimbali na kasi kubwa ya mabadiliko ya teknolojia yanayotokea duniani na kuhitaji Maafisa TEHAMA kujengewa uwezo mara kwa mara ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

 Changamoto nyingine ni kutofanyika kwa vikao vya Kamati za TEHAMA za taasisi (‘ICT Institutional Steering Committee’) kwa wakati kama inavyoelekezwa katika Sheria ya Serikali Mtandao, ambapo athari yake ni kuwepo kwa mifumo ya TEHAMA ndani ya Taasisi ambayo haijibu mahitaji ya Idara zote husika ndani ya Taasisi, hivyo kutokuwa na tija iliyokusudiwa.

Serikali ina malengo ya kuimarisha utawala bora na kuongeza tija na ufanisi katika uendeshaji wa taasisi za Umma kwa kuhakikisha kuwepo kwa mawasiliano ya haraka, yenye uhakika na salama  kati ya taasisi mbalimbali za Serikali,vilevile amewataka taasisi za umma kuzingatia Ulinzi wa taarifa binafsi na kuhakikisha pia taasisi imesajiliwa na tume ya ulinzi wa taarifa binafsi. 

Akitoa salam za mkoa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Toba Alnason Nguvila amesema kuwa, mkoa wa Arusha ni wadau wa matumizi ya Serikali huku Taasisi zote za binafsi na Serikali mkoani huo, zikitumia mifumo ya kidijitali katika kutoa huduma kwa wananchi, lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali na dhamira ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya kidijitali katika kutoaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Nguvila amebainisha kuwa, Mamlaka ya Serikali Mtandao - eGA, ni wadau wa kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa Taasisi za Serikali nchini ambapo Mkoa wa Arusha ni wadau wakubwa wa Serikali Mtandao, kutokana na kuwa Taasisi zote za Serikali mkoani humo, ni watumiaji wazuri wa mifumo ya kidigitali kwa kuzingati ndio sera na maelekezo ya Serikali.

Akitoa salam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar, Dkt. Said Seif Said, amesema wataendelea kushirikiana na Serikali Mtandao Bara kuboresha huduma, huku Mwenyekiti wa Bodi ya e-GA, Mussa Kissaka, akieleza kuwa mkutano huo unalenga kukusanya maoni yatakayosaidia kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa njia ya kidijitali.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 inayofanya kazi ya kuimarisha na kuendeleza utoaji wa huduma za serikali mtandao kwa taasisi za Umma ,lengo ni kuziwezesha Taasisi hizo kutumia TEHAMA katika majukumu yao ili kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

No comments