Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Sharon Sauwa Afariki Dunia

DODOMA

Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi, Sharon Sauwa, amefariki dunia ni alfajiri ya August 19,2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila.

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma, Yusuph Mussa, aliyesema Sauwa alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu kabla ya umauti kumkuta.

“Kwa masikitiko makubwa dada yetu mpendwa Sharon amefariki dunia leo majira ya alfajiri akiwa katika matibabu Hospitali ya Mloganzila. Ameugua kwa muda mfupi na kwa kweli ni mipango ya Mungu,” amesema Mussa.

Sauwa, ambaye amekuwa mwandishi wa habari wa siku nyingi, amehusiana na habari za siasa na bunge kwa muda mrefu, akijipatia heshima na umaarufu mkubwa miongoni mwa wanasiasa, wanahabari na wasomaji.

No comments