PROF.KABUDI :WAANDISHI EPUKENI HABARI ZA KUGHUSHI
Prof.KABUDI :WAANDISHI EPUKENI HABARI ZA KUGHUSHI
Na Vero Ignatus Arusha.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Paramagamba Kabudi amewataka waandishi wa habari kuepuka habari za kugushi, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ili kuepuka kupotosha umma au kuleta taharuki.
Prof. Kabudi ametoa pongezi kwa waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuhabarisha umma kuhusu taarifa mbalimbali za serikali, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Nishati uliohudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali, uliofanyika jijini Dar es Salaam, na akawasihi waendelee kuelimisha wananchi kuhusu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani hiyo ni ajenda ya kitaifa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Saida Muki, amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na matumizi ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI) wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili wasiwasilishe maudhui yanayoweza kupotosha umma.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Grayson Msigwa, amewashauri waandishi wa habari kuwa, kupitia Mkutano huu, wanapaswa kuzingatia weledi katika taaluma yao hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kulinda usalama wa taifa.
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari, akizungumza katika mkutano huo Jijini Dodoma Leo 13 machi 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari, amesema mkutano huu umeandaliwa ili kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya habari na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokikabili sekta hiyo.
No comments