TEKNOLOJIA YATAJWA KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KUBORESHA NA KUTUMIA KUIMARISHA UIMBAJI WA KWAYA KANISANI.

TEKNOLOJIA YATAJWA KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KUBORESHA NA KUTUMIA KUIMARISHA UIMBAJI WA KWAYA KANISANI. 

Katika picha ni kwaya ya Rita wadogo Mtakatifu Rita wa Kashia  katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, wakiwa katika muonekano huo wakiimba katika utambulisho wa wimbo maalum wa Tawala Bwana

Prof. Joseph Nduguru Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Arya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ambaye pia ni Mlezi  wa Mtakatifu Rita wa Kashia  katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, 

Katika picha ni kwaya ya Rita wadogo Mtakatifu Rita wa Kashia  katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, wakiwa katika muonekano huo wakiimba katika utambulisho wa wimbo maalum wa Tawala Bwana

Prof. Joseph Nduguru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ambaye pia ni Mlezi  wa Mtakatifu Rita wa Kashia  katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, akiwa na Rita Wadogo. 

TEKNOLOJIA YATAJWA KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KUBORESHA NA KUTUMIA KUIMARISHA UIMBAJI WA KWAYA KANISANI. 

Na. Vero, Ignatus Arusha

Uwepo wa teknolojia kumetajwa kuleta mapinduzi makubwa katika uimbaji wa kwaya makanisani, na kuleta faida nyingi na msaada mkubwa katika kuhifadhi kumbukumbu na nyimbo mbalimbali tofauti na hapo awali karatasi na Daftari zilikuwa zikitumika jambo ambalo halikuwa salama. 

Prof. Joseph Ndunguru ni Mlezi wa kwaya ya Mtakatifu Rita wa Kashia  katika Parokia ya Mtakatifu Yuda Tadei, akizungumza hivi karibuni katika Uzinduzi wa wimbo maalum wa  Tawala Bwana alisema wanahitaji shilingi Milioni 50 kwaajili ya kununia vifaa vitakavyowasaidia katika kuhubiri na kurahisisha huduma ya uinjilishaji

Aidha Prof. Ndunguru alisema kuwepo kwa vifaa vya kisasa husaidia upanuzi wa wigo wa huduma,  Uhifadhi wa kumbukumbu, Uboreshaji wa ubora wa sauti,vile vile inasaidia kuhifadhi historia ya kwaya na kurithisha nyimbo na mila kwa vizazi vijavyo 

Ameitaka jamii na waumini kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kwaya mbalimbali kwa jumbe zinazoimbwa zinaweza kubadilisha maisha ya watu wengine na kuwainua waliovunjika mioyo na kupiga hatua nyingine. 

"Tunahitaji Kupata kinanda kidogo, spika power mixer, Umplifire, tumba, pamoja na vishkwambi kwaajili ya matumizi ya nota ya nyimbo tunazoziimba Mara kwa Mara kanisani".

Jonas Aloyce Ngowi ni mwenyekiti wa kwaya hiyo Malengo ya 2025 ni kukusanya million hamsini kwaajili ya akiba ya kwaya kupata kinanda kidogo tumba mixer pamoja na spika kwaajili ya kwaya kwaajili ya matumizi ya kwaya pamoja na vishkwambi 25 kwaajili ya misa na kwaya 

Ngowi mesema Kutokuwa na hivyo vifaa kumekuwa na changamoto Kwenye uinjilishaji kwani Mara nyingi wanatumia karatasi ambapo Mara nyingi zinapotumika au kulowa zinachakaa na kupotea 

Ngowi Amesema kuwa matarajio yao bado wanaendelea kuu za flashi kwaajili ya kuongeza kipato cha kwaya kutembelea Parokia na sehemu mbalimbali kwaajili ya kuinjilisha na kufanya mauzo ili kufikia lengo kwaaliki ya shughuli mbalimbali za kwaya hiyo alisema utambulisho wa wimbo huo umekwenda sambamba na Uzinduzi wa Rita Charity pamoja na kutambulisha mfumo Mpya wa kurekodi nyimbo za Injili. 

Alisema kuwa kwaya hiyo inapambana kutoa huduma bora za kuinjilisha,matendo ya huruma ,majitoleo kwa kutumia njia za kisasa zinazogusa watu wa zama hizi bila kuharibu tungo za miziki wala kuharibu tungo za miziki na misingi ya Kikatoliki. 


No comments