Makonda:Umuhimu wa Afya huduma bora,Kwa wamama wajawazito pamoja na wenye matatizo ya moyo kupatiwa vipimo na tiba stahiki.


Makonda:Umuhimu wa Afya huduma bora,Kwa wamama wajawazito pamoja na wenye matatizo ya moyo kupatiwa vipimo na tiba stahiki. 
Na. Vero Ignatus, Arusha
Katika  Kuelekea siku ya wanawake duniani 8machi 2025 ambayo itafanyika Kitaifa mkoani Arusha ,Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,  Paul christian  Makonda, ameongoza kikao kazi cha maandalizi ya maadhimisho ya Siku hiyo , akisisitiza umuhimu wa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, watoto, na wenye matatizo ya moyo.
Makonda amesisistiza kuanzia tarehe 1/2/2025-7/2/2025 kutakuwepo na shughuli mbalimbali zitakazofanyika ikiwemo utoaji wa huduma, elimiu, kuonyesha kazi zilizofanyika, Michele, huku akiwasisistiza wakiu wa wilaya pamoja na wakirugenzi wa Halmashauri kuwataafifu wananchi wao ili waweze kwenda kwenye mkitano kwaajilo ya kitatua migogoro iliyoshindikana kutoka kwenye wilaya. 
Aidha kikao hicho, kimewakusanisha viongozi viongozi mbalimbali wa sekta za Serikali na ya afya na mashirika yanayojihusisha na ustawi wa jamii walihudhuria, wakisisitiza mshikamano katika kuboresha huduma za afya kwa wanawake nchini.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya kIkwete (JKCI) Dk, Peter Kisenge, ambaye alieleza mipango iliyowekwa kuhakikisha wanawake na watoto wanapata huduma bora za uchunguzi wa afya.
"Tumepanga kuhakikisha kina mama wajawazito wanapimwa afya zao, watoto pia wanahakikishiwa huduma bora, na vilevile wale wenye matatizo ya moyo wanapata vipimo na tiba stahiki. Hii ni dhamira yetu katika kuhakikisha afya ya wanawake inalindwa."


No comments