SERIKALI:MKOA WA ARUSHA UMEPOKEA JUMLA YA SH BIL 79 KWAAJILI YA SEKTA YA ELIMU.

Na.VERO IGNATUS ARUSHA

SERIKALI:MKOA WA ARUSHA  UMEPOKEA JUMLA YA SH BIL 79  KWAAJILI YA SEKTA YA ELIMU. 

Serikali imesema kwa kipindi cha miaka mitano Iliyopita Mkoa wa Arusha umepokea jumla ya shilingi bilioni 79 kwaajili ya sekta ya elimu ambapo kiasi cha shilingi  bilioni 25 ni kwaajili ya miundombinu ya miradi ya elimu, shilingi bilioni 54 kwaajili ya elimu bila malipo.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari julai 8 Jijini Arusha na kwamba   katika kipindi hicho  jumla ya vyumba vya madarasa    810   yenye thamani ya bilion  16.2 vimejengwa na kufanya mkoa  katika shule za  sekondari kuwa na jumla ya madarasa 3,093

Akizungumzia juu ya abiria wanaoingia nchini Msigwa amesema kwa rekodi za 2022/23 KiA imeweza kuhudumia zaidi ya abiria 900,000 ambapo kwa mwaka 2019/20 uwanja ulihidumia abiria 720,000 hiyo ni kwa  mujibu wa tafiti zinazofanyika ambapo  abiria wanaoshuka katika uwanja wa kimataifa wa kia kwa  60%ni watalii

Aidha serikai imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kushirikianana wadau kwa kujenga uwanja wa kia  ambao unafanya vizuri, kwani  kwa sasa kuna ndege;10 za kimataifa  zinazotua katika uwanja huo

Amesema  katika mkoa wa Arusha yapo majengo ya kisasa 4 kwaajili ya huduma za dharura EMD katika hospitali ya rufaa  ya Mountmeru Karatu, Ngorongoro sambamba na wodi mbili za wagonjwa mahutihuti (ICU)Mountmeru na Longido.
 
Aidha mkoa wa Arusha una huduma ya dharura wa mika mitano iliyopita serikai imeongeza huduma za kutolea matibabu kitoka 383 hadi kufikia vituo 42 halmashauri zote saba za mkoa zina hospitali zenye hadhi ya wilaya. 

"Serikali imeweza kukarabati vituo vya Afya 25 zahanati 45 na vyumba vya watumishi 26 katika mkoa wa Arusha "Alisema

Msigwa alitoa ufafanuzi juu ya ndege ya Airbus 220 iliyoliyokuwa imeshikiliwa nchini Uholanzi iliyokuwa chini ya sheria tayari serikali imeshafanya mazungumzo julai 7tayari ndege hiyo imerudi nchi.

Akizungumza juu ya ujazaji maji katika Bwawa la umeme la Julius Nyerere la mto Rufiji amesema kuwa inaendelea kwakiwangi kilichopangwa cha kufikia mita 163 juu ya usawa wa bahari ambapo tayari maji yameshafikia januari 2024 inawezekana ujazo wa maji ukafikia ujazo wa mita 184 ambapo majaribio yanatarajiwa kuanza februari 2024 na mwezi juni uzalishaji rasmi utaanza. 

No comments