.DKT.SAMIA:JANGA LA RUSHWA MOJA YA VIKWAZO BARANI AFRIKA .NI MIONGONI MWA MAKOSA YANAYOVUKA MIPAKA
NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
.DKT.SAMIA:JANGA LA RUSHWA MOJA YA VIKWAZO BARANI AFRIKA
.NI MIONGONI MWA MAKOSA YANAYOVUKA MIPAKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia
Suluhu Hassan amesema serikali imeweza kuokoa kiasi na kuthibiti matumizi ya
fedha yasiyostahili Zaidi ya shilingi bilioni 139 kuanzia mwaka wa fedha
2019/20hadi 2021/22 kwa kupitia divisheni ya mahakama kuu inayosikiliza kesi za
washtakiwa wa makosa ya rushwa kubwa.
Amesema hayo katika kilele cha maadhimisho ya mapambano
dhidi ya rushwa Barani Afrika na Maadhimisho ya utekelezaji wa miaka 20 ya Mkataba
wa Umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa kwamba viongozi wote hawana budi kuimarisha
mapambano na Dunia itambue kuwa Afrika siyo salama kwa wala rushwa
‘’ Nataka niwaelezee kwa kifupi safari ya
Tanzania katika utekelezaji wa mkataba huu,sisi Tanzia tulisaini novemba 5,2003
na kuridhia 22februari 2005 na tulianza kuutumia rasmi tarehe 5Agosti 2006 ,leo
Tanzania ni miongoni mwa nchi 48 kati ya nchi 55zilizosaini na kuuridhia
mkataba huu na tumekuwa tukiadhimisha siku hii tangu mwaka 2018,kufuatia uamuzi
wa umoja wa Afrika Julai 2017 ulifanya 11julai kuwa siku ya kupiga vita rushwa’’Alisema
Mhe.Samia.
‘’Tanzania ilitunga sheria ya kupambana na rushwa
no 11mwaka 2007 ambapo sheria hii ndoiyo iliyoanzisha Taasisi ya Kuzuia na
kupambana na Rushwa na kujumuisha pia makosa ya rushwa yanatotajwa katika
mkataba wa Umoja wa Mataifa 2003 na nchi ipo katika mchakato wa kufanya mapitio
ili iendane na wakati tulionao’’Alisema Rais
Aidha Mhe.Samia amesema moja ya vikwazo barani Afrika
ni janga la rushwa vitendo hivyo ni miongoni mwa makosa yanayovuka mpaka,katika
mjadala ulioondelea umeonyesha kuwa baadhi ya makundi yanayoongoza kwa rushwa
ni Jeshi la Polisi,Wanasiasa,vyuo vya elimu ya juu,Mahakama na wafanyabiashara hivyo
ni vyema wakajitathmini na kujirekebisha.
Samia amesema serikali imejiwekeza katika matumizi ya mifumo ya tehama inayosaidia kupunguza
mawasiliano ya ana kwa ana katika kutoa huduma kama michakato ya zabuni usajili wa biashara nan
amba yam lipa kodi ili kupunguza mianya ya rushwa.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais katiba,sheria,utumishi
na utawala bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema rushwa inaumiza
wanyonge na inaumiza kila mahali hivyo kila mmoja kwa upande wake ashiriki
vyema vita dhidi ya rushwa,ambapo wanategemea siku moja Afrika kuwa huru kutoka
kwenye janga la rushwa
Suleiman amesema
kuwa wanatarajia kuja na mbinu mpya katika mapambano dhidi ya rushwa,kwani Zanzibar
imepitisha sheria bora ya mapambano dhidi ya rushwa ,hivyo kupitia maadhimisho
hayo Afrika nzima itakuwa na msimamo mmoja katika mapambano dhidi ya vita hii
ya rushwa.
Akizungumza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru CP.Salum Rashid Haamduni amesema kuwa Maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa hufanywa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika zilizosaini na kuridhia AUCPCC,ambapo ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba huo ambapo madhumuni yake ni kutafakari mapambano dhidi ya rushwa
‘’ Makosa ya dawa za kulevya mara nyingi huchochewa na uwepo wa vitendo vya rushwa’’ alisema Hamduni
No comments