AICC KULETA MAPINDUZI YA UTALII WA MIKUTANO, KWA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA UWEKEZAJI CHA MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER (MKICC)
AICC KULETA MAPINDUZI YA UTALII WA MIKUTANO,
KWA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA UWEKEZAJI CHA MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER
(MKICC)
NA.VERO IGNATUS,ARUSHA
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC chini ya Ushirikiano
wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wanayodhamira
kubwa ya kuweza kuleta mapinduzi ya utalii wa mikutano,kwa kujenga kituo
kikubwa kitakachoitwa Mount Kilimanjaro International Convention Center (MKICC)kitakachokuwa
na ukumbi wenye ukubwa wa kubeba wageni 3000, eneo la maonyesho lenye uwezo wa
kuchukua watu zaidi ya 10,000 pamoja na eneo watakalowekeza hoteli za Kitalii.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa AICC Efraim Mafuru
amesema tayari wanalo eneo Site D1 la
heka 90 zenye umbali wa kilometa 2 amesema lengo lao ni kulibadilisha matumizi
na wataanza kwa kujenga hoteli moja ya
nyota tano,japo mpango wao ni kuwa na hoteli mbili za nyota tano zenye uwezo wa
kuchukua wageni zaidi ya 1000,ambapo wataanza ujenzi mwaka huu wa fedha.
‘’Tutaendelea kuwekeza katika kumbi kubwa za kisasa ili
Tanzania iweze kushindana ,sasa hivi kama mnavyojua tulikuwa wa 11 katika
Afrika miaka 4 iliyopita lakini ndani ya miaka 2ya uongozi wa serikali ya awamu
ya 6 Tanzania imepanda hadi nafasi ya 5,lakini mimi nasema dhamira yetu ni
kuingia tatu bora ndani ya muda mfupi’’Alisema Mafuru
Mafuru amesema kuwa kwa kuzingatia mchango wa Economic Diplomacy
ili kuweza kuwaleta wadau waliopo katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii
wa mkutano watawekeza pia katika shopping Mall kubwa ili wafanya biashara
waweze kuja kuuza bidhaa zao kwa wageni wanaokuja katika mikutano
‘’Mbali na hivyo tunaamini kwamba ili kuweza kuwahudumia
viongozi wakuu wan chi tutaweka maeneo maalum ambayo tutatoa taarifa baadae
yatakavyokuwa lakini hata tukiweza kuwa na viongozi zaidi ya 15-20 kwa kwa
wakati mmoja tuweze kuwahudumia,na kutimiza dhamira na ndoto ya Mhe.Samia
Suluhu ya ya kufanya Tanzania kitovu cha utalii wa mikutano itatekelezwa katika
kiwanja hiki’’Alisema Mafuru.
Kwa upande wake msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa
aliipongeza AICC kwa mapango wao huo na kusema Serikali inautazama mkoa wa
Arusha kama mkoa wa kimkakati na Kwenda na ndoto yake ya kuifanya Tanzania kuwa
kitovu cha utalii Barani Afrika na inahitaji mchango mkubwa na sauti ya pamoja kutoka
kwa wadau
‘’kumekuwa na tabia Fulani kwamba mambo makubwa na mipango kama
hii inapotaka kufanyika kuna vikundi vya watu vinatengeneza fitna ,hebu tuache
fitna mafanikio yoyote ya kiuchumi yanataka uwekezaji,na lazima ushirikiane na
sekta binafsi,kwahiyo watanzania mtuelewe kwasababu tunataka makusanyo ya
mapato yanayotumika naserikali tuyatumie Kwenda kutoa huduma kwa watanzania ,mfano
uwekezaji wa kituo kikubwa cha uwekezaji ni biashara’’Alisema Msigwa.
Msigwa amesema ilani ya CCM imewaelekeza kufikia watalii mil
5 ifikapo mwaka 2025,ambapo kwa sasa wameanza Kwenda vyema mwaka 2022 waliweza
kufikia watalii mil 1.5,ambapo wanaweza kufikia watalii mil 2kwa kipindi kifupi
kijacho kwani safari bado inaendelea kwaajili ya kufikia idadi hiyo ya wageni.
Amewataka Watanzania kuelewa kwamba wanapokwenda kwenye
uwekezaji mkubwa kama huo Serikali inaangalia kwa karibu na kuangalia maslahi
ya Taifa,ukiangalia mwaka 2022 AICC wameingiza mapato ya Bil 17 ,ambapo
wanasema wakiwekeza wanaweza kufikia hadi bil 40-100
‘’Tutoke kwenye mapato madogo tunayoyapata twende kwenye
mapato makubwa kwa kutumia style za kisasa za uwekezaji na haya mambo
yanawezekana,lazima tuingize mawazo mapya yanayokuja kutuletea mageuzi na
maendeleo’’Alisema Msigwa.
No comments