WAZIRI JAFO:MAZINGIRA YAKIHARIBIWA UCHUMI NAO UNAYUMBA
| Mratibu wa miradi midogo UNDP Faustine Ninga akipokea nakala ya kitabu toka kwa Dr. Jaffo |
| Afisa utawala wa Maipac Andrea Ngobole,ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa habari Fanikiwa kilichopo kwa Mrombo Jijini Arusha akipokea nakala ya kitabu toka kwa Dr. Jaffo |
WAZIRI JAFO:MAZINGIRA YAKIHARIBIWA UCHUMI NAO UNAYUMBA
NA: VERO IGNATUS, ARUSHA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr. Seleman JafFo amezindua kitabu cha kwanza maarifa ya asili katika uhifadhi wa Mazingira ,misitu na Vyanzo maji,ambapo siyo yale ya sayansi na teknolojia za mazingira bali hutokana na uzoefu wa simulizi
Kitabu kilichozinduliwa kimeandikwa na Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) Kwa kushirikiana na taasisi ya CILAO kimetokana na simulizi za wazee la Mila ya kimasai, wanawake na vijana wa jamii hizo katika wilaya za Ngorongoro, Longido na Monduli,kwani jamii hiyo wamekuwa ikiendeleza ikiendeleza mila na desturi katikamaisha yao ya kila siku.
Dr. Seleman Jafo amesema uhifadhi wa mazingira kwa maarifa ya asili ni muhimu kwani , kwani maarifa hayo yalikuwa yanatumika toka enzi za mababu ambapo imesaidia kutunza misitu, vyanzo vya maji na mazingira, kitabu hicho kitakuwa njia sahihi ya kueneza elimu ya utunzaji wa Mazingira kwa njia ya asili.
"Mazingira yakiharibika na maisha /uchumi unaharibika,Huu ni mradi wa kwanza wa aina yake nawapongeza MAIPAC Kwa kazi nzuri kwani pia nimeona documentary nzuri na Nina Imani UNDP na wafadhili wengine wataendelea kuwapa fedha zaidi kuendeleza mradi "nawapongeza kwa kutoa kitabu cha utunzaji wa mazingira kwa maarifa ya asili.alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC Mussa Juma amesema kuwa kitabu hicho ndani yake kimeelezea simulizi za jamii ya Maasai wanavyotumia taratibu na mila zao katika kutunza vyanzo vya maji, misitu na mazingira kwa ujumla huku wazee wa kimila maarufu kama Laigwanani wakiwafundisha vijana namna bora kuheshimu mila na desturi zao hususani katika kutunza mazingira,vyanzo vya maji na misitu.
''Mradi huu ulizinduliwa rasmi Agosti 27,2022 jijini Arusha na Mkuu wa mkoa wa Arusha, ambaye aliwakilishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa Arusha''.
Musa alisema kuwa Amesema Mradi huo umefadhiliwa na programu ya miradi midogo ya mfuko wa mazingira Duniani(GEF) unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) nchini Tanzania chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais –Idara ya Mazingira.
Afisa maendeleo ya jamii mkoa Arusha Bi. Blandina Nkini ameipongeza MAIPAC kwa kuwa shirika pekee lililokuja na mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili na kuwa moja ya shirika la mfano mkoani Arusha kati ya mashirika 1114 yaliyosajiliwa mkoani Arusha na kuwaomba wafadhili wengine kuwasaidia katika kutekeleza miradi yao.
Mratibu wa miradi midogo UNDP kupitia shirika la mfumo wa Mazingira duniani (GEF) Faustine Ninga ameipongeza MAIPAC kwa kukamilisha kuchapa vitabu na kuandaa video na machapisho ya mradi huo.
Katibu wa baraza la mila la kimasai Tanzania Amani Lukumayi ameipongeza MAIPAC kwa kuandaa kitabu cha aina yake kinachoelezea umuhimu wa maarifa ya asili katika uhifadi wa mazingira, utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu kwani utakuwa urithi muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha lengo kuu la kitabu hicho ni kwaajili ya kubainisha maarifa asili yanavyotumika katika masuala ya uhifadhi wa mazingira ,utunzaji wa vyanzo vya maji ,uhifadhi wa misitu na katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi miongoni mwa jamii ya za Maasai zinazoishi kaskazini mwa Tanzania.
Sambamba na hayo kitabu hicho kimetokana nautekelezaji wa mradi wa utunzaji wa mazingirabkwa kutumia maarifa ya asili uliofadhiliwa na program ya Small Grants ya mfuko wa mazingira duniani (GFF) unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Nchini Tanzania,chini ya uratibu wa mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais -Idara ya Mazingira.
No comments