TRA YAWATAKA WAMILIKI WA MABASI NCHINI KUZINGATRIA MABADILIKO YA SHERIA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI
Steven Athanas-Meneja Elimu kwa Mlipakodi TRA Makao makuu,akitoa ufafanuzi kwa kwaandishi wa habari.
Said Sharifu, Katibu mtendaji wa AKIBOA ambaye ameshiriki semina hiyo:kanuni zinazotungwa kwa lugha ya kingereza siyo rafiki kwao.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku moja yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia kwa makini kile kilichokuwa kikitolewa ufafanuzi katika ukumbi wa Golden Rose Jijini ArushaTRA YAWATAKA WAMILIKI WA MABASI NCHINI KUZINGATRIA MABADILIKO YA SHERIA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI
Na VERO IGNATUS, ARUSHA
Mamlaka ya Mapato nchini TRA imewataka wamiliki wa mabasi nchini kuzingatia Mabadiliko ya Sheria katika Sekta ya Usafirishaji pamoja na mfumo wa utoaji Tiketi kwa njia ya Mtandao ili kuiwezesha Serikali kuingiza mapato sahihi.
Steven Atanas, Meneja wa Elimu na Huduma kwa mlipakodi TRA,Meneja wa Elimu na huduma kwa mlipakodi akizungumza jijni na wadau wa sekta ya usafirishaji mkoani ARUSHA ambaye amesema iwapo wakitumia mfumo huo vizuri matokeo chanya yataonekana
Atanas amesema tangu mabadiliko ya sheria za kodi zimebadilika julay 2022 pamekuwa na malalamiko kwa wanaotakiwa kutekeleza sheria hizo hivyo wakaona ni vyema kuwapa elimu.
"Mabadiliko ya sheria yamefanyika ili kuboresha utendaji wa kazi na
kurahisisha ukusanyaji wa mapato lakini kama wahusika hawatakuwa na uelewa na mabadiliko hayo tutabaki kusumbuana tu" amesema Atanas.
Salum Pazi, Kaimu Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, amesema fursa ya kukutana kwao inasaidia kupata maoni ambayo yatatumika kufanya maboresho ya namna ya utendaji kazi kwa pande zote kwa siku zijazo.
Salum Pazi amesema matumizi ya Tiketi mtandao yatasaidia wasafirishaji kwa njia ya mabasi na kuepukana na upotevu wa mapato sahihi katika shughuli zao.
Kwa upande wake Mabula Sambayuka, Meneja wa EFD, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, amesema lengo la semina hiyo ni kuwahimiza wafanyabiashara hao ili waweze kukuza mapato ya nchi kupitia tiketi mtandao mtandao.
Naye Said Sharifu, Katibu mtendaji wa AKIBOA ambaye ameshiriki semina hiyo amelalamikia kanuni zinazotungwa kwa lugha ya kingereza ambayo si rafiki kwao,huku wakiiomba Serikali kutoa mafunzo mara kwa mara
Semina hiyo iliwakutanisha wa wamiliki wa mabasi, Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na wadhibiti wa usafiri ardhini.
No comments