KUKITHIRI KWA MIGOGORO YA ARDHI YATAJWA KUWA CHANZO KIMOJAWAPO CHA MAUAJI -ARUSHA

Baadhi ya Majaji wakiwa katika maadhimisho ya wiki ya sheria yakiyofanyika katika Mahakama kuu kanda ya Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika Mahakama kuu kanda ya Arusha
Jaji Mfawidhi kanda ya Arusha Mosses Mzuna ,Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya sheria  2/2/2022,
Baadhi ya  Mawakili wa serikali pamoja na Mawakili wa kujitegemea wakiwa katika maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika Mahakama kuu kanda ya Arusha
Baadhi ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA wakiwa wameshiriki maadhimisho ya wiki ya sheria mkoani Arusha 2/2/2022 yaliyofanyika Mahakama kuu Kanda ya Arusha

KUKITHIRI KWA MIGOGORO YA ARDHI YATAJWA KUWA CHANZO KIMOJAWAPO CHA MAUAJI -ARUSHA

Na.Vero Ignatus,Arusha

 Majaji na Mahakimu wametakiwa  kuwa na utu katika mashauri mbalimbali wanayosikiliza na kuyatolea maamuzi, pamoja na kupinga  vitendo vya rushwa ambayo ni adui wa haki,ambapo wiki hiyo imekwenda  sambamba na mwaka wa kazi  Kimahakama wa mwaka 2022

Hayo yamesemwa na Jaji Mfawidhi kanda ya Arusha Mosses Mzuna ,Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya sheria  2/2/2022,ambapo aliekemea mambo yanayotokea mkoani humo  ikiwemo kukithiri kwa mauaji kwa wanafamilia au jamii, ambayo baadhi hutokana na migogoro ya ardhi,ubomoaji wa majengo/ nyumba bila amri halali, wakati kuna mashauri yanaendelea  mahakani,pamoja na  kutumia madalali ambao hawajasajiliwa.

Mzuna  alisema kumekuwa na  kitendo cha kuchelewa kwa upelelezi wa mashauri na  kuchukua muda mrefu, jambo ambalo husababisha  kudhoofisha kasi ya usikilizwaji wa mashauri kwa wakati,Ambapo amesema  tatizo hilo lisipotibika hawataweza kutimiza malengo ya kumaliza mashaurikwa wakati,hivyo amezitaka ofisi zinazohusika lisimamie jambo hilo

Aidha amesema changamoto ambayo wanakabiliana nayo ni pamoja na wanafamilia kutokufungua mashauri ya mirathi mahakamani kwa wakati, hivyo kuchochea migogoro ya kifamilia na hatimaye kupelekea mashauri ya msingi kuchelewa,pia  jamii kutokutumia njia ya usuluhishi kama njia mbadala hadi h,upekelea kufikishana mahakamani hata kama suala ni dogo

‘’Ardhi isiwe sababu ya kusababisha hadi sisi wana arusha kuuwana jamani ,halafu mnasubiria siku ya mahakama ndipo mnakwenda kuvunja kweli?msiwasababishe majaji na mahakimu waonekane hawana maamuzi sahihi, Harutakubali majaji na mahakimu simameni katika haki wasiwepo watu kukuonyesha wewe kesi ipo mahakamani lakini anakuja kuvunja simameni kidete katika hili’’Alisisitiza Jaji Mzuna

Kwa upande wake mkuu wa mkoa John Mongela ameupongeza uongozi wa mahakama ya Arusha kwa kazi kubwa inayofanyika katika wiki nzima iliyopita, kwa kujihusisha na jamii kwa kutoa msaada wa kisheria ,kwani kulikuwa na  baadhi ya mambo yalikuwa katika ofisi yake ambapo baadhi wananchi wametoa shuhuda, kwamba wamefahamu jambo gani wafanye ili kupata haki zao.

Mongella alisema kuwa jambo hilo limenawasaidia  mihimili mingine katika kuhakikisha kunakuwa na utulivu kwa jamii,kwani kazi kubwa inayofanywna mahakama inachangia kwenye majukumu yao ya kiutendaji,pamoja na kuhakikisha   usalama na utulivu kuwepo ,hivyo ameahidi kuwa karibu na mahakama pale wanapohitajika na kuhakikisha kwamba mhimili huo unakuwa imara zaidi.

Kwa upande wake wakili wa serikali mfawidhi aliyeiwakilisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Veritas Mlay alisema katika kuelekea mahakama ya mtandao katika zama za mapinduzi ya nne ya viwanda inaondoa mipaka kati ya utaratibu ulikuwa umezoeleka kwa muda mrefu wa mtu kuzoeleka kuwepo mahali Fulani kimwili na kutumia utaratibu wa kidigitali wa matumizi ya tehama

Amesema kwa upande wa mahakama 2015-2016 iliweka azma Madhubuti ya kuweka marekebisho makubwa katika mfumo wa matumizi ya tehama kwa ujumla,aidha hatua ya maboresho kuelekea mahakama ya mtandao ilikolea Zaidi mwaka 2018 ambapo Jajimkuu wa Tanzania alitoa kanuni ya ufunguaji mashauri kwa njia ya mtandao kupitia tangazo la serikali no 148 ambazo zimewezesha mashuri kufunguliwa masaa 24.

Amesema mabadilio ya maisha na ufanyaji biashara  na mambo mengine yanayotokea katika Maisha ya mwanadamu kipekee yanakwenda sambamba na huduma ya utoaji haki,hivyo huduma za utoaji haki hazina budi kuendeshwa kwa njia ya kimtandao  

Amesema mapinduzi hayo yan ne yameongeza ufanisi kuanzia pale matumizi ya kwanza hadi ya tatu yalipofikia ambapo mapinduzi ya kwanza yalitokea katika karne ya 18 ambapo binadamu aligundua mashine ya kuwezesha uzalishaji kwa mara ya kwanza duniani,ya pili yalileta ugunduzi wa mafuta ya nishati na umeme pamoja na maendeleo mengine ya kisayansi,mapinduzi ya tatu yalianza 1950 ambapo vya tehama kama tarakishi viligundulika

Kwa upande wake mwenyekiti wa mawakili wa kujitegemea George Njooka alisema kuwa tasnia ya sheria iangalie kwa kina juu ya bongo bandia (Artificial Teligency) ielekezwe kwenye kuelewa ubongo wa binadamu na kuchakata matumizi yakuwa sahihi na bora ya tehama ili kubresha utoaji haki kwa wananchi na kutatua changamoto zinazoikabili jamii

Alisema kuwa kukua kwa bongo bandia kunaweza kuleta maendeleo kwa utoaji wa haki nchini hivyo sekta hiyo haina budi kujizatiti na kujiandaa kufanya maandalizi mwananaili muda ukifika maboresho ya utoaji haki na ushauri ya kisheria uelekezwe kwenye usahihi wa taarifa na sheria husika ili haki ya mwananchi ionekane kufanyika kwa muda mfupi

Alihitimisha kwa kusema kuwa ili waweze kwenda kwa kasi katika kuleta maboresho kuelekea mahakama mtandao inahitajika kuhakikisha kuwa jamii inakubaliana na hayo ya kutegemea bongo bandia na matumizi ya tehama katika utoaji haki sambamba na elimu ya kutosha itolewe ili mapokezi yake yawe chanya .

Mwisho

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments