WAZAZI NA WALEZI TUWAJUZE VIJANA WETU JUU YA MABADILIKO YA KIMWILI NA NAMNA YA KUYAKABILI ILI TUWAJENGE KITABIA NJEMA


Na.Vero Ignatus,ARUSHA

Ni kawaida katika ukuaji wa mwanadamu kupitia katika Vipindi mbalimbali ambavyo katika kila hatua yapo mabadiliko atakayoyaona Kimwili na Kama asipoweza kuendana na mabadiliko hayo yanaweza mbadilisha Tabia na kupelekea kuongezeka Kwa uhatari wa Kubadilika Kwa Tabia zake na hasa Tabia hatarishi.
 
Mabadiliko hayo ni yale ya Kibaiolojia,Kimwili na Kisaikolojia na mwisho hufika katika hatua ya ukomavu wa Kibaiolojia na Uwezo wa kuzalisha(fertility) kwa maana ya yai(ovum) Kwa wanasichana na Mbegu za kiume(sperm) Kwa wavulana

Kwa kawaida kati ya kipindi cha Utoto na Kipindi cha Utu uzima Kuna Kipindi cha Balehe kipindi ambacho una mabadiliko ya Kimwili,kitabia na kimtizamo kwa pande zote za kike na kiume sana kutokana na vichocheo ndani ya miili ya Vijana hawa ambavyo huzalishwa ndani ya miili Yao na hapa ndipo Kundi Kubwa hubadilika kitabia na kuanza michezo ambayo ina uhatari kwa Afya zao 

Kwa Upande wa Jinsia ya Kike wengi huanza kuona mabadiliko hayo Kati ya Miaka 9 Hadi 11  japo wapo wanaowahi chini ya Miaka 9(precocious puberty)na na wapo wanaochelewa Hadi kufikia Miaka 16(delayed Puberty) mabadiliko hayo Kukamilika Hadi Miaka 16 

MABADILIKO YA VICHOCHEO(ENDOCRINOLOGY IN PUBERTY)

Mabadiliko mbalimbali yanayotokea huambatana na mabadiliko ya ki Homoni hasa katika Homoni zinazozalishwa katika Ubongo na Ovari (Hypothalamopituitary gonadal axis) ambayo hupelekea Homoni mbalimbali kuzalishwa mwilini 

Imekuwa kawaida Kwa Vijana Wengi kutokuelezwa na walezi ,wazazi au Jamii wanayoishi kama shule juu ya mabadiliko haya na kuwapelekea kushindwa kuyakabili 
 
Ipo dhana imejengeka kuwa mama au mlezi wa kike kimweleza mtoto juu ya mabadiliko ya Kimwili na kihomoni ni kumfundisha jambo ambalo sio sahihi lazima kama Jamii tuwekane sawa tukijua kuwa Kuna mimba za utotoni ,Kuna Maambukizi ya virisi vya Ukimwi,Kuna magonjwa ya Zinaa ikiwepo Homa ya Ini aina B(Hepatitis B) na magonjwa Mbalimbali

Mabadiliko Kwa upande wa Kiume nayo ni Hivyo hivyo kuchagizwa na Mabadiliko ya Kihomoni na huathiri Sana Tabia za vijana Wetu

Ili tujenge Taifa la kesho Imara lazima tuwapike kuanzia utotoni, matokeo ya Vijana werevu,wenye maadili yasiyoyumbishwa na mabadiliko ya Kimwili hutengenzwa kuanzia utotoni
 
Leo hii tunapozungumzia ukubwa wa Maambukizi ya Virus vya Ukimwi kundi Kubwa la Vijana ndio wahanga wa hili Kati ya Miaka 18-24 .
 Tunapozungumzia suala la Mimba za utotoni,Tunapojadili suala la matumizi ya madawa ya Kulevya , matumizi ya Vilevi , Magonjwa ya Akili na Kisaikolojia na kupelekea Mauaji ya wanajamii na Matendo Mengine yasiyo ya kawaida kundi Kubwa linalohusika na Lile la Miaka 17-30 ambalo Athari ya Matendo yake yamekuwa ni ya kutisha katika jamii Yetu

Kupitia mchango Mkubwa wa viongozi wa dini zetu zote hakika Maadili ya Vizazi vyetu yatabaki kuwa Bora milele na Kwa MAPENZI yake Mungu Kizazi Cha Taifa hili la Mungu kitaendelea kuwa Bora na BORA
 
Kipekee Niwapongeze Viongozi wa dini ambao wamekuwa Nguzo muhimu wa MAFUNZO kama haya Kwa watoto na Vijana wetu hakika ni jambo jema Sana ambalo Linapaswa kufanywa maeneo mbalimbali, MUNGU AWALIPE KILA LILILOJEMA

Ndugu Zangu Wakati Tunaendelea kufurahia Uzima na UHAI aliotupa Muumba wetu tukumbuke maneno yafuatayo

Nchi na vyote vijazavyo ni Mali ya Bwana ,Dunia na wote wakaao
Zaburi 24:1

Pia katika Quran suurat Al-Faatih'a 

Aya ya Pili,Tatu na Nne Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu,Mola Mlezi wa Viumbe vyote

Hivyo tuishi ya kuwa Tukikumbuka kuwa sote sisi ni wa MWENYEZI MUNGU na ili tuendelee kutekeleza Mafundisho na maagizo Tunapaswa kuwaletea watoto na Vijana wetu katika malezi yatakayompendeza MUNGU ili Kwa PAMOJA TULIJENGE TAIFA

Credit to;
*DR JUMA MUNA*
0789602283/0655809171
Jumamuna924@gmail.com

No comments