JUKWAA LA WAKULIMA ARUMERU LAPATA NEEMA

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa mmoja wa mkulima katika maonyesho ya wakulima wilayani hapo. 
 DC Muro akizungumza na wakulima katika maonyesho hayo ya kilimo yaliyoanza tarehe 1-3 Novemba 2018 wilayani humo. 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wakulima na wananchi wa wilaya hiyo katika maonyesho hayo ya wakulima
 Mmoja kati ya mkulima. Wilayani humo akimpatia maeleza ya mbegu ya mahindi kama inavyoonekana katika picha Mkuu wa wilaya Jerry Muro katika maonyesho hayo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiwa katika picha ya pamoja na wakulima katika maonyesho hayo ya wakulima Meru. 

Na. Vero Ignatus, Arumeru. 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amejitolea  kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze kukopesheka na Ta asisi za kifedha 

Amesema hatua hiyo imefikia baada ya kubaini kuwepo kwa vikwazo katika maandiko katika hatua za awali kwani Taasisi hizo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo, andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

 Wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa vikwazo hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi  kuondoa Vikwazo hivyo.

Mhe Muro amesema tayari kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima (PASS)Private Agricultural Sector Support imekubali kuwaandalia na kugharamia Mpango kazi wa kibiashara zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara. 

Akifungua maonyesho ya jukwaa la wakulima Meru ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo kwa pamoja  wamekukubali kutoa msaada katika kuandaa, kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara 

Muro amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji Jukwaa hilo la Wakulima Meru  ili kuwawezesha kufanya kazi zao Kwa haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia kompyuta Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za taarifa za wakulima na wafugaji.

Kwa upande Meneja wa Tawi la kampuni ya ( PASS)amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo. 

Mwisho. 

No comments