TANZANIA YAPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA BARABARA
Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuboresha ujenzi wa barabara kwa kutumia Teknolojia ya kuchanganya lami Kulingana na Mazingira husika katika kanda mbalimbali Nchini na ipo teyari kwa ajili ya uwekezaji kwa maendeleo ya uchumi wa taifa .
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele katika mkutano wa kimataifa Mhandisi amesema wakala wa barabara nchini Tanroads wameanzisha miongozo ya kuchanganya lami Kulingana na Mazingira ya hali ya hewa ya mikoa mbalimbali ili kuweza kujenga barabara imara zitakazoendana na mazingira husika.
Ameleza kuwa Tanzania kutokana na mikutano hiyo wameweza kufanikiwa kutengeneza Teknolojia mpya ya kuchanganya lami kutokana na mazingira na jiografia ya maeneo ambapo mfano lami inayojengwa Katavi itaendana na hali ya hewa ya Mazingira yake ili barabara zisiharibike na kudumu kwa muda mrefu hivyo kusaidia kukuza uchumi.
Amewata wataalamu wa TANROADS kutofanya kazi Kwa mazoea na pia kuhakikisha wanatatua matatizo ya sehemu zao za kazi wasisubiri hadi mamlaka za juu kuwapangia majukumu yanayowahusu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA Deusdedit Kakoko akiongea kama mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni sehemu muhimu kwao kama mamlaka ya bandari wamejipanga kutumia mkutano huo kuboresha utendaji wao wa kazi
Kuangalia mabadiliko ya teknolojia ya usafirishaji na matumizi ya Tehama yatasaidia kuboresha na kubadilika kwa kwenda kwenye kizazi cha nne cha mapinduzi ya usafirisha duniani ambapo jambo hilo litaharakisha utoaji wa bidhaa katika bandari .
Kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Mapinduzi ya nne ya sekta ya usafirishaji yanayohusiana na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea.
Mwisho.
No comments