UMOJA WA ULAYA(EU) WAKABIDHI VIFAA KWAAJILI YA MAABARA YA KISASA TAEC

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala   akizungumza na Meneja Mredi kutoka Jumuiya ya nchi za Ulaya Genevieve Liz pamoja na wageni wengine alioonhozana nao. 
Denis Mwalongo Mkuu wa Idara ya Mionzi, mashine za kuhakiki vifaa vya mionzi katika mwili wa binadamu akiwaonuesha wageni hao kutoka Umoja wa Ulaya jambo 
Dkt Wilbroad Muhogora mwenye (shati la draft) Mtafiti wa Tume akifafanua jambo kwa wageni kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na, waandishi wa habari

Na, Vero Ignatus Arusha 

Umoja wa Ulaya (EU) umerithishwa na ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) ikiwemo uwekaji wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh, bilioni 2.3. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo, Meneja Mradi na Usalama wa Masuala ya Mionzi, kutoka EU, Genevieve Lizin alisema umoja huo umerithishwa na kazi nzuri ya uwekaji vifaa uliofanywa na serikali. 

Alisema Umoja huo umeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kudhibiti masuala ya mionzi ndio maana wametoa ili kudhibiti masuala ya mionzi katika nchi za Afrika. 

"Maabara hii ni ya kisasa na hakuna mfano wake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hivyo tumeridhika na kazi waliyofanya Taec katika zoezi la uwekaji vifaa ambavyo sisi tumevitoa "

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Lazaro Busagala  alisema serikali imetoa Sh, bilioni 2.3 kwaajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kwa lengo la kuhakikisha maabara hiyo inatoa huduma bora za kisasa za masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika. 

Aidha alishukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya Sh, bilioni 11.5 vilkvyofungwa kwenye maabara za Tume hiyo ambavyo vimetolewa na Umoja wa Ulaya (EU)

Alisema  serikali kwa awamu ya kwanza imetoa Sh, bilioni 1  huku fedha nyingine Sh, bilioni 1.3 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa ambayo itaweza kutumiwa na watu mbalimbali nchini na nchi za Afrika 

"Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha maendeleo ya nchi yanasonga haswa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu serikali "

Katika maabara hiyo kutakuwa na uhakiki wa vifaa vya kupimia mionzi, chumba cha mionzi mikali kwaajili ya kupikia vyuma kwa njia ya kupiga picha kwa kutumia mionzi pamoja na chumba cha kutumia mionzi kwaajili ya shughuli nyingine ambamo kitasimikwa kifaa cha kupima viasili vya mionzi vilivyopo mwilini mwa binadamu. 

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kupima mionzi iliyoko ndani ya Mwili wa binadamu (whole body counter), mashine ya kuhakiki vifaa vya mionzi , Secondary standard dosimetry laboratory ( SSDL)

Mashine ya kupima viasili vya mionzi kwenye mazingira , maji na hewa TXRF, mashine ya kupima mionzi kwenye vyakula aina ya Hyper pure Germanium detector. 

Sambamba na mashine ya kupima mionzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mazingira ya vyanzo vya mionzi inayoitwa Harshaw 6600

Mwisho

No comments