THABIT KOMBO AWASILI ARUSHA KuSHIRIKI MKUTANO 3 WA TUME YA PAMOJA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA NA UCHUMI KATI YA TANZANIA NA URUSI
ARUSHA:
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Tatu ngazi ya Mawaziri kuhusu Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara kati ya Tanzania na Urusi.
Kombo amewasili leo Mei 14, 2026 kupitia Uwanja wa Ndege wa Arusha na kuungana na mawaziri wengine wanaoshiriki mkutano huo, Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Ngwaru Maghembe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dk. Pius Chaya, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.
Mkutano huo umeanza Mei 12, 2026 kwa ngazi ya Wataalam na sasa unaendelea kwa ngazi ya Mawaziri, huku Hati za Makubaliano (MoU) kadhaa zikitarajiwa kusainiwa kwa pande zote mbili za Tanzania na Urusi.
Credit Habari Leo
No comments