RIPOTI YA JAJI CHANCE INA HOJA MUJARABU TUSIPONDE KWA KUFUATA MKUMBO
Katika kile kinachoonekana kama msisitizo wa dhati wa kulinda uhuru na utu wa taifa, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ametoa wito mzito kwa Watanzania kuamini na kutumia mifumo yao ya ndani katika kutatua migogoro badala ya kukimbilia msaada kutoka kwa mataifa ya nje.
Jaji Chande amebainisha hayo hivi karibuni akitoa ufafanuzi jinsi ripoti yake iulivyofanyakazi na methodoliojia ya kisayansi iliyotumia kuypata majibu katika kadhia iliyoitia doa nchi hapo Oktoba 29 mwaka 2025.
Katika ufafanuzi wake alifundisha bayanakuwa dhana ya kutafuta wageni kuja kuingilia mivutano ya ndani ni ishara ya kutojiamini na kupuuza busara ambazo Watanzania wamezitumia kwa miongo mingi kudumisha utulivu.
Amesisitiza kuwa kama taifa hatujashindwana na tuna uwezo kamili wa kuketi meza moja na kumaliza tofauti zetu bila kuhitaji "macho ya nje" ambayo mara nyingi hayajui undani wa utamaduni na mshikamano wetu.
Uchambuzi wa ujumbe huo unaonesha kuwa amani ya kweli inajengwa juu ya msingi wa haki na usawa ambapo kila raia, bila kujali cheo chake, anapaswa kujiweka chini ya sheria.
Aidha, katika ripoti yake amesisitiza matumizi ya njia mbadala za kutatua migogoro kama vile usuluhishi na upatanishi ambazo hupunguza chuki na mivutano ndani ya jamii.
Amesisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuamini mifumo ya kisheria iliyopo kwani ndiyo njia pekee ya kulinda fahari ya nchi. Kwa mujibu wa Jaji Chande, uongozi wenye maono na hekima ni ule unaoweza kujifunza kupitia makosa ya nyuma na kuimarisha amani kama chaguo kuu la taifa, huku akihitimisha kuwa amani yetu ni fahari yetu na ni jukumu la kila mmoja wetu kuilinda kwa gharama yoyote.
@@@@@@@@@@@@@
Tukumbushe Machungu ya Oktoba 29: Kwanini Ripoti ya Jaji Chande ni Dawa ya Kudumu ya Kulinda maisha ya Watanzania
Ujumbe wa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman unapaswa kupokelewa kama msingi imara wa mustakabali wa nchi yetu, tukikumbuka madhila mazito yaliyowasibu wananchi kufuatia machafuko na fujo zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.
Tukio hilo liliacha kovu kubwa katika mioyo ya Watanzania wengi kutokana na kusimama kwa shughuli za kiuchumi na kijamii, ambapo wafanyabiashara walikosa wateja na sheli za mafuta zilifungwa, hali iliyosababisha usafiri kuwa wa shida na gharama za maisha kupanda ghafla.
Hakuna Mtanzania anayetamani kurejea katika kipindi kile ambacho hata mahitaji ya msingi kama chakula yaligeuka kuwa anasa, huku bei za bidhaa kama mchele, unga, na nyanya zikipaa kiasi cha nyanya mbili tu kuuzwa hadi shilingi elfu moja, jambo lililoumiza familia nyingi mitaani kwetu.
Athari hizo hazikuishia kwenye uchumi pekee, bali zilivuruga kabisa mfumo wa huduma za kijamii na kuwanyima watoto wetu haki yao ya msingi ya kupata elimu ndani ya siku hizo za taharuki.
Shule zilifungwa na mazingira ya kupata huduma za afya yakawa magumu, jambo linalothibitisha kuwa uvunjifu wa amani haubagui na badala yake unarudisha maendeleo ya taifa nyuma kwa miaka mingi.
Kwa kuzingatia machungu hayo, ni wazi kuwa ushauri wa Jaji Chande wa kutaka tutumie mifumo yetu ya ndani kusuluhisha migogoro ni wa busara kubwa, kwani fujo hazileti katiba mpya wala tume huru, bali zinaleta umaskini, njaa, na uharibifu wa mali za wananchi wanyonge ambao wamejitafutia kwa jasho lao.
Hivyo basi, huu ni wito kwa vijana na wananchi wote kwa ujumla kukataa kutumika katika harakati zozote za uvunjifu wa amani ambazo mwisho wake ni hasara kwa taifa na maumivu kwa mtu mmoja mmoja.
Tunapaswa kuwa macho na vishawishi vinavyoweza kutuingiza katika fujo zinazokusudiwa kurudisha nyuma ukuaji wa biashara na ustawi wa jamii yetu.
Ni wajibu wetu sote kulinda utulivu tulionao kwa sababu bila amani hakuna biashara itakayostawi, hakuna mtoto atakayesoma, na gharama za maisha zitaendelea kuwa mzigo mkubwa kwa mwananchi wa kawaida.
Tuungane kuienzi ripoti ya Jaji Chande kama dira ya kisheria na ya kizalendo ili kuhakikisha kuwa madhila ya Oktoba 29 hayajirudii tena katika ardhi ya Tanzania.
No comments