MAKAMU WA RAIS AWASILI ARUSHA, KUUFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA TAPSEA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Jumatano Mei 20, 2026 amewasili Mkoani Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, tayari kwaajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA).
Mhe. Mkude katika mapokezi hayo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Dkt. Toba Alnason Nguvila pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM na wa serikali.
Mkutano wa TAPSEA unafanyika Alhamisi Mei 21, 2026 katika ukumbi wa Tanzania Convention Centre (TCC) ulioko Ngurdoto Mountain Lodge, Arumeru ukiwa na kaulimbiu isemayo "Ubunifu, uwajibikaji, uadilifu na ufanisi ni mojawapo ya misingi imara ya maendeleo endelevu kwenye utendaji kazi."
No comments