ARUSHA, TANZANIADKT JACOB JULIUS ROMBO AZINDUA RASMI HOSPITALI YAKALOLENI NGAZI YA WILAYA
Na Vero Ignatus,Arusha
Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Dkt Jacob Julius Rombo leo amezindua rasmi Hospitali ya Kaloleni ngazi ya wilaya jijini Arusha kufuatia Kituo cha Afya Kaloleni kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ngazi ya wilaya kupitia maboresho makubwa yanayoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na mamia ya wananchi, viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu wa afya waliojitokeza kushuhudia hatua hiyo muhimu katika kuboresha huduma za afya ndani ya Jiji la Arusha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt Rombo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha amesema Serikali imeendelea kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za kisasa karibu na maeneo yao.
Amesema kupandishwa hadhi kwa Kituo cha Afya Kaloleni na kuwa Hospitali ya Wilaya kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za matibabu pamoja na kupunguza changamoto kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kufuata huduma mbali na
maeneo yao.
Aidha amewapongeza wataalamu wa afya kwa juhudi wanazoendelea kuzifanya katika kuwahudumia wananchi huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujituma kwa maslahi ya wananchi.
Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo wakisema ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya
No comments