WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI.
WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI.
Na. Vero Ignatius Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za mauaji ya Omary Mnandi (30) Askari Polisi Mkazi wa Jiji la Arusha.
Akitoa taarifa hiyo leo Oktoba 12, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo amesema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Oktoba 12, 2025 muda wa usiku huko katika Bar iitwayo Simaloi iliyopo maeneo ya Kaloleni Jijini Arusha.
SACP Masejo amebainisha kuwa watuhumiwa hao walimjeruhi mhanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea umauti wake wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha.
Aidha, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya Omary Mnandi (marehemu) kutokana na unywaji wa pombe ambao ulipelekea kukosea uhakika wa gari lake Na. T. 402 CNC na kuingia kwenye gari Na. T. 734 AXR la mmoja wa watuhumiwa hao na ndipo walianza kumshambulia.
Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linakamilisha uchunguzi wa tukio hilo ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe.
No comments