RAIS wa Kenya, William Ruto ameongoza shughuli ya kuuaga mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Nchi hiyo, Raila Odinga
RAIS wa Kenya, William Ruto ameongoza shughuli ya kuuaga mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Nchi hiyo, Raila Odinga katika uwanja wa Kasarani, Jijini Nairobi akiwa ameambatana na familia ya Mwanasiasa huyo mkongwe aliyepoteza maisha Oktoba 15, 2025 nchini India alipokuwa akipokea matibabu.
Mwili wa Hayati Odinga umeonekana ukiwa kwenye Jeneza lililofunguliwa ukiwa umevalishwa kitambaa chenye rangi ya machungwa kikiashiria chama alichokiasisi na kukiongoza kwa takariban miaka 20 chama cha Orange Democratic Party.
Vilevile aliyekuwa Rais wa nne wa Nchi hiyo Uhuru Kenyatta pia amehudhuria shughuli hiyo iliyoanza kwa maombi kutoka kwa Viongozi wa kidini.
Haya yanajiri baada ya purukushani kutokea katika Uwanja huo kufuatia wafuasi wa Raila kujaa pomoni Uwanjani huku Polisi wakiwatawanya waombolezaji na kwa sasa hali imekuwa tulivu wakibaki waombolezaji wachache uwanjani.
No comments