TAEC:IPO KWENYE MCHAKATO WA UANZISHWAJI WA MRADI WA UTUNZAJI WA VYAKULA KWA TEKNOLOJIA YA MIONZI

"Juni 28,2023,tulipokea mswada ambao ulisomwa  Bungeni kwa mara ya kwanza na mswada huo ni washeria mbalimbali wa mwaka 2023 ambapo miongoni mwa sheria sita ambazo zinarekebishwa katika mswada huo ni sheria inayoiguza Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzani "
Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo,Profesa, Lazaro Busagala,Akizungumza Jijini Arusha wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya  Utawala ,Katiba na  Sheria iliyotembelea Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)Kanda ya Kaskazini Arusha
Pichani ni Kamati ya Kudumu ya  Utawala ,Katiba na  Sheria iliyotembelea Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)Kanda ya Kaskazini Arusha
Pichani ni Kamati ya Kudumu ya  Utawala ,Katiba na  Sheria iliyotembelea Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)Kanda ya Kaskazini Arusha

TAEC:IPO KWENYE MCHAKATO WA  UANZISHWAJI WA MRADI WA UTUNZAJI WA  VYAKULA  KWA TEKNOLOJIA YA MIONZI


NA VERO IGNATUS,ARUSHA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala, Katiba na Sheria ,imesema kuwa imeanza mchakato wa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ili kuipa nguvu ya kisheria Tume ya Nguvu za Atomic Tanzani(TAEC)

Hayo yamesemwa hivi karibuni  na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ,Florient Kyombo  wakati wa ziara makao makuu ya  TAEC ambapo  alieleza kuwa ziara hiyo imelenga utekelezaji wa maazimio ya bunge, katika kuchakata mswada wa mabadiliko ya sheria ikiwemo inayoigusa tume kiutendaji

Aidha  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge,Utawala,Katiba na Sheria,Florent Kyombo aliipongeza TAEC kwa kudhibiti mionzi isilete athari kwa binadamu sanjari na vyakula sambamba kumpongeza Rais,Dk, Samia Hassan Suluhu kwa kutoa zaidi ya sh, bilioni 10 kwaajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa kutoa fursa mbalimbali za tafiti zinazohusiana na matumizi ya nyuklia.

"Rais Samia tunampongeza kwakuweka ulinzi madhubuti wa kudhibiti mionzi isilete athari kwa wananchi lakini pia TAEC inatoa huduma mbalimbali za kiutafiti katika kuhakikisha mionzi haileti athari kwa wananchi na vitu vinginevyo "

Akizungumza Jijini Arusha wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya  Utawala ,Katiba na  Sheria iliyotembelea Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)Kanda ya Kaskazini, Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo,Profesa, Lazaro Busagala alisema TAEC ipo kwenye mchakato wa uanzishwaji mradi wa vyakula kutunzwa kwa njia ya mionzi ,ambapo alisema njia hiyo ni salama zaidi kuliko vile vinavyotunzwa kwakutumia kemikali. 

Profesa Busagala amesema Wakulima wa zao la vitunguu wataweza kunufaika na teknolojia ya mionzi katika kuhifadhi mazao na vyakula visiweze kuharibika mapema na kuchochea uchumi wa viwanda ikiwemo ongezeko la pato kwa wakulima.

Alisisitiza kuwa uhifadhi wa vitunguu kwanjia ya mionzi unachukua miaka mitatu bila kuharibika na  mradi huo unatekelezwa katika Nchi 62 Duniani na kwa upande wa Afrika zipo nchi 6 ambapo Tanzania itakuwa ni nchi ya saba kutekeleza mradi huo kwa Afrika pale utakapokamilika.

"Teknolojia ya mionzi ni salama zaidi kuliko kuhifadhi kwanjia ya kemikali,itakapoanza itakuwa na manufaa zaidi kwa wakulima sanjari na uhifadhi wa chakula lakini pia itakuwa mkombozi kwa wakulima na kujikwamua kiuchumi"Alisema Prof. Busagala.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo,Edward Lekaita(Mb. Kiteto) alisema ziara yao katika kituo hicho ni kujionea utendaji kazi wa tume  ili kuridhia mabadiliko ya sheria yaliyoombwa na TAEC. 

"Nia yetu kuja hapa ni kuona na kulinganisha yale ambayo TAEC wanataka bunge litunge sheria ,kamati imejiomea na kujua baadhi ya vitu ,tumebaini hii ni taasisi muhimu sana inayoshughulikia masuala nyeti ya afya za watu na sisi kama wajumbe tutaenda kulishauri bunge"alisema Lekaita.

Naye mbunge wa Busanda ,Tumaini Magesa,alisema elimu walioipata TAEC ni vizuri ikatolewa pia kwa wananchi  ili kuwasadia uelewa juu ya athari za mionzi kwenye chakula na manufaa yake.

"Sisi kama wabunge hatuwezi kupitisha sheria bila kujiridhisha ,hivyo uwepo wetu hapa umetusaidia kuielewa TAEC na shughuli zake, tumetembelea takribani maabara  12 na tumeona uwezo wa tume na tutaenda Kulishauri bunge"


Mwisho

No comments