ASSAD:WAJUMBE WA BODI WAPATIKANE KWA KUAJIRIWA
Msajili wa hazina Nehemiah Mchechu, akizungumza katika Kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji wakuu wa Taasisi za Umma leo August 19 Jijini Arusha
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mstaafu ,Profesa Mussa Assad akizungumza na wshiriki wa Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha. Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe akizungumza na washiriki wa Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano AICC leo Jijini Arusha. •Tunatamani iwe inafanyika kila mwaka oia kujua kwa kazi tunazofanya pamoja na kuzungumza changamoto za kiutendaji na kijifunza kitoka kwa wenzetu waliofaulu" "Msajili wa hazina Nehemiah Mchechu.
ASSAD:WAJUMBE WA BODI WAPATIKANE KWA KUAJIRIWA
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mstaafu ,Profesa Mussa Assad ameshauri Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma nchini,wapatikane kwa kuomba kazi na kufanyiwa usaili ili kujenga umakini zaidi.
Ameyasema hayo wakati akitoa mada juu ya Uendeshaji wa Mashirika ya Umma na tafakuri kuhusu Tanzania,Leo Agosti 19,katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha(AICC) kwamba upatikanaji wa wajumbe wa bodi ni tatizo hivyo no vyema jambo hilo lizingatiwe.
Profesa Assad amesema ili bodi za Mashirika ya Umma kufanya kazi kwa ufanisi ni lazima wajumbe wanaopatikana wawe uwezo wa kusaidia Taasisi na sio kuwa mzigo kwa taasisi za Umma.
'Siyo anateuliwa mtu anakuja kwenye Bodi kisha kikao kikiwa kinaendelea yeye hachangii jambi lolote lile akiulizwa anasema nimekuja kujifunza, kisha mwisho wa siku kikao kikimaizika anadai bahasha'
Aidha amesisitiza kuwa matatizo mengine yanayotokea au yaliyopo kwenye Mashirika ya Umma, Bodi,ni pale watendaji wa mashirika kuingiliwa na viongozi juu wa Serikali na hivyo kutolewa maamuzi ambayo yanaathiri mashirika.
Profesa Assad amesema pia kuna Matumizi mabaya ya fedha za Mashirika ikiwepo ununuzi wa magari ya kifahari ikiwepo V8 ya mwaka 2023 na Kila Mtendaji wa Serikali kuwa na magari hayo.
"Kuna haja gani kuwanunuliwa watendaji watano katika Taasisi Moja magari matano ya kisasa V8 ambapo inabidi kuajiri madereva,lazimamaeneo ya kuegesha magari"amesema
Amesema sio Kila wakati maafisa hao wote watakuwa safarini wakitumia magari hivyo inapaswa kuwa na magari machache hatamatatu na watendaji wakatumia kwa zamu.
"Lakini pia kuna hili nimeona tunakuja Arusha kwenye mkutano watendaji na wanakuja na ndege na magari yanawafata Arusha ili waje kutembelea nadhani hii pia ni matumizi mabaya ya Rasilimali za Mashirika "amesema
Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe ameshauri kuwa Wizara ibakie na masuala ya Kisera na siyo masuala ya Kiuendeshaji pamoja na
Kabwe amesema ni vyema kuimarisha na kuitazama upya sheria ya mashirika ya Umma, na kuona jinsi gani wataona mashirika yanavyoajiri kulingana na uwezo wao wa kiutendaji.
Mwisho
No comments